Sunday, August 25

Hakuna mipaka tena katika mawasiliano

0


Kampuni
ya Halotel Tanzania imekuja na huduma mpya ya mawasiliano iitwayo
‘MPANGO MZIMA’ ambayo pamoja na faida zake nyingine inamuwezesha
mtumiaji wa simu wa mtandao wa Halotel kupata unafuu katika huduma
mbalimbali za simu.

Kuanzishwa
kwa huduma ya Mpango Mzima ni muendelezo wa kampeni mbalimbali
zinazoendelea kufanywa na Halotel katika kumrahisishia mteja wake kupata
huduma bora za mawasiliano zikiwemo za kutumia Intaneti bila kikomo,
kupiga simu matandao yote bila kikomo, kutuma ujumbe mfupi wa
maneno(sms), 

Akiziungumza
kuhusu ‘Mpango Mzima’ Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son alisema
ujio wa huduma hiyo mpya na ‘Kijanja’ imelenga kumwezesha mtumiaji wa
mtandao huo kutumia intaneti yenye kasi na ukubwa wa (GB 5) bila kikomo.

Pamoja
na Intaneti hiyo mtumiaji wa mtandao huo pia ataweza kupiga simu kwenda
mitandao yote bure kwa kila dakika 5 za kwanza pamoja kuzawadiwa sms
5000 atakazozitumia katika kipindi cha mwezi mzima.

“Huu
ni muendelezo wa mpango wa mapinduzi ya kimawasiliano wa Halotel kuwa
karibu na kuwajali wateja wetu kwa huduma bora. Kuanzishwa kwa Mpango
Mzima kutamwezesha mteja wetu wa Halotel kutumia intaneti ya kasi kubwa ,
kupiga simu bila kikomo kwa mitandao yote bure kila dakika 5 za mwanzo
na hivyo kumuondolea hofu ya simu kukatika kabla hajamaliza maongezi”
amesema Son.

Amesema
ili mteja aweze kufaidika na huduma hiyo mpya anapaswa kujiunga kwa
kupiga *148*66# na kuchagua Mpango Mzima ambapo ataweza kujiunga na kuwa
tayari kwa kuanza kufurahia unafuu huo mahususi kwa ajili ya watumiaji
wa mtandao wa Halotel.

Mkurugenzi
huyo Bw. Nguyen Van Son amesema huduma ya Mpango Mzima ni mpya kuwahi
kutolewa na mtandao mwingine wowote wa simu hapa nchini na kuwaambia
watumiaji wa Halotel kuwa hiyo ni zawadi kwao hivyo wanapaswa kuifurahia
na kuitumia wakati wote.

Aidha
Mkurugenzi huyo Bw. Nguyen Van Son wa alisema Halotel pia imeweza
kuunganisha Optic Fiber zenye urefu wa zaidi ya Kilomita 20,000 katika
maeneo yenye miundombinu yake kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa data
kwa maeneo mapya na hivyo kuiwezesha kuwa chaguo la kwanza kwa wateja
pale linapokuja suala la huduma za Internet.

Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo, Mhina Semwenda. (kulia)
akionesha jinsi mteja anavyoweza kujiunga na huduma ‘Mpango Mzima’
katika uzinduzi wa huduma hiyo ambayo inatoa unafuu kwa watumiaji wa
mtandao huo katika matumizi ya Intaneti na kupiga simu bila kikomo
mitandao yote kwa kila dakika 5 za mwanzo kwa mwezi mzima. Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Nguyen Van Son.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Halotel, Nguyen Van Son (kulia) akizungumza na waandishi wa
habari katika uzinduzi wa huduma mpya ijulikanayo kama ‘Mpango Mzima’
ambapo inatoa unafuu kwa watumiaji wa mtandao huo katika matumizi ya
Intaneti na kupiga simu bila kikomo mitandao yote kwa kila dakika 5 za
mwanzo kwa mwezi mzima. Uzinduzi huo ulifanyika katika ofisi za Halotel
Makao Makuu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha
Mawasiliano wa kampuni hiyo, Mhina Semwenda.

Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo, Mhina Semwenda. (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa huduma mpya
ijulikanayo kama ‘Mpango Mzima’ ambapo inatoa unafuu kwa watumiaji wa
mtandao huo katika matumizi ya Intaneti na kupiga simu bila kikomo
mitandao yote kwa kila dakika 5 za mwanzo kwa mwezi mzima. Uzinduzi huo
ulifanyika katika ofisi za Halotel Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Nguyen Van Son

Share.

About Author

Leave A Reply