Saturday, August 17

ELIMU YA AFYA YA UZAZI BADO NI CHANGAMOTO KWA WASICHANA NA VIJANA

0


Pamella Chogo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya “Chanya Change”akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)

Anna Mahenge Mtaalamu wa Masuala ya Afya ya uzazi anasema familia nyingi zimekuwa zikishindwa kukaa na mabinti zao na kuwaeleza ukweli kuhusu afya uzazi 

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Kutokana na asilimia kubwa ya wasichana na vijana kutokuwa na uelewa juu ya Afya ya uzazi jamii kuanzia ngazi ya familia zimetakiwa kuwajengea uwezo ikiwa ni sehemu ya kuwaelimisha kuhusiana na afya ya uzazi katika maisha ya kila siku,

Taasisi ya Kimataifa ya “Chanya Change”imeendelea kutoa elimu ya kujitambua na kuchukua tahadhari kutokana na vihatarishi katika mazingira wanayo ishi wasichana zaidi ya 100 katika shule mbalimbali katika jiji la Arusha wakiwa na lengo la kuwasaidia kujitambua ,kutoa hamasa katika masomo ya sayansi pamoja na mafunzo ya Tehama kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo 

Akizungumza na Michuzi Blog Pamela Chogo ambae ni muandaaji wa warsha hiyo iliyo andaliwa na taasisi ya Kimataifa ya “+Chanya Change” kwa ajili ya wasichana amesema Msichana ana nafasi kubwa katika kuchochea shughuli za kimaendeleo ya taifa hususani katika Masuala ya Sayansi na teknolojia (TEHAMA) 

Amesema jamii inatakiwa kuondokana na mtazamo hasi kuhusu watoto wa kike kwamba hawawezi kufanikisha mambo,badala yake watambue wanawake wengi wamekuwa wakutumia changamoto hiyo Kuwa fursa katika jamii wanazo ishi hatimae wameleta chachu ya Maendeleo kuelekea Tanzania ya Viwanda.

“Ni wakati muafaka kwa jamii kuondokana na mtazamo Hasi kuhusu mtoto wa kike Kuwa hawezi kufanikisha Mambo muhimu katika jamii,mwanamke ndio msingi wa maendeleo”alisema Pamela.

Amesema bado kumekuwa na wimbi kubwa kwa baadhi ya wasichana kuto jitambua kutokana na kukosa elimu ya Afya ya uzazi kwa Vijana ngazi ya familia hivyo wazazi wanajukumu kubwa la kuelimisha Watoto wao wa kike wakaribiapo Rika la balehe ili kuepukana na ongozeko la ndoa,mimba za utotoni.

“Wazazi wengi bado wanatamaduni za kizamani ambazo zimekuwa chanzo Cha wasichana wengi kujiingiza Kwenye makundi Hasi yanayo pelekea kupata magonjwa na Matumizi ya madawa ya kulevya kwa kukosa elimu ya jinsi”

Anna Mahenge ni mtaalamu wa Masuala ya Afya ya uzazi anasema familia nyingi zimekuwa zikishindwa kukaa na mabinti zao na kuwaeleza ukweli kuhusu afya uzazi jambo ambalo limekuwa likichangia ongezelo la vihatarishi na maambukiIi ya magonjwa ya zinaa pamoja na mimba za utotoni.

“Kuficha ficha mambo kwa wazazi juu ya wasichana kuhusu maumbile na maungo ya uzazi bado ni Changamoto kwa jamii, hivyo jamii ibadilike”alisema muuguzi huyo.

Nao baadhi ya wasichana waliowashiriki katika warsha hiyo wamesema Asasi za Kiraia zinazo hudumia jamii waige mfano wa kinacho fanywa na taasisi ya Chanya Change ili kufika katika maeneo husika na kutoa elimu ili kukiandaa kizazi chanya kwa siku zijazo.

Share.

About Author

Leave A Reply