Saturday, July 20

ZIARA YA JUKWAA LA WANAWAKE WILAYA YA MKURANGA YAJA NA FURSA YA MKOPO BILA RIBA

0


Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MWENYEKITI
wa Jukwaa la wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega ameendelea na
ziara yake iliyolenga kuhamasisha kuwainua wanawake kiuchumi kupitia
jukwaa hilo.

Akizungumza na wanawake akiwa ziarani katika kijiji
cha Mwandege bi. Mariamu amesema kuwa lengo la kufanya ziara hiyo
kuwafahamisha wanawake kuhusiana majukumu yanayofanywa na jukwaa hilo
tangu kuanzishwa kwake.

Amesema kuwa akiwa kama mweyekiti wa
Wilaya hiyo atahakikisha fursa za kiuchumi zinawafikia ili waweze
kuendeleza shughuli zao za kijasiriamali.Kuhusiana na mikopo kwa
wanawake bi. Mariamu amesema kuwa wanachotakiwa kufanya ni kuendeleza
miradi yao ili waweze kupata mikopo katika halmashauri zao bila riba.

Kwa
upande wake diwani wa kata ya Mwandege Adolf Kowero amesema kuwa
amekuwa akifarijika na juhudi za akina mama hao na kuhusu ahadi ya eneo
alilohaidi kwa ajili ya biashara lipo tayari na ramani imeandaliwa
ambapo soko kubwa litajengwa kwa ajili ya wanawake na vijana.

Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega
akizungumza na wajasiriamali wa kata ya Mwandege ,ambapo amewaomba
kufanya kazi kwa waminifu ili waweze kunufaika na kazi zao na kuongeza
pato la Taifa.
Diwani wa kata ya Mwandege wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani,Adolf Kowero akizungumza na wajasiriamali wa kata hiyo.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya Mkuranga,Mariam Ulega
akiwakabidhi viongozi wa kata ya Mwandege laki nne na doti 20 za kanga
kwajili ya mtaji wa vikundi mbalimbali vya kata hiyo.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya Mkuranga,Mariam Ulega akiwaunga
mkono wajasiriamali wa kata ya Mwandege.(Picha na Emmanuel Massaka MMG)
Sehemu ya wajasiriamali wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika kata ya Mwandege wilayani Mkuranga Mkoani wa Pwani.

Share.

About Author

Leave A Reply