Sunday, August 18

Waziri wa Afya ashiriki kwenye ungawaji wa vyandarua ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani

0


Waziri wa Afya ashiriki kwenye ungawaji wa vyandarua ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani

Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu,amesema kuwa Serikali imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa
Malaria kwa asilimia 50 kutoka asilimia 14 mwaka 2015 hadi kufikia
asilimia 7.

Hayo ameyasema leo wakati wa kugawa vyandarua kwa
wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu katika hospitali ya
Wilaya ya Dodoma.

Aidha,amesema kuwa halmashauri kutenga fedha
za ndani kwa ajili ya kununua viuwadudu ikiwa ni katika kupambana na
maambukizi ya Malaria katika maeneo yao.

Waziri Ummy amesema
kuwa kwa kipindi cha miaka 2 ya utawala wa Rais John Magufuli, Tanzania
imeweza kupunguza maambukizi ya Malaria kwa asilimia 50 kutoka wastani
wa asilimia 14 mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 7.

Hata hivyo
amesema kuwa serikali imekuwa na mikakati mingi ya kupambana na
maambukizi wa ugonjwawa malaria ambayo yamekuwa ikiuwa Watanzania wengi
kuwa mbali na kugawa vyandarua pia wanapulizia dawa katika mikoa yenye
kiwango kikubwa cha maambukizi.

”Serikali imenunua takribani
lita 60,000 ya viuawadudu kwa ajili ya kuua mazalia ya mbu na kuzigawa
katika mikoa yenye maambukizi makubwa ya malaria kama vile Mkoa wa
Kagera, Geita, Kigoma, Lindi na Mtwara lakini pia niwaombe wananchi
kutunza mazingira ili kujiepusha na mbu waenezao malaria,” amesisitiza
Mwalimu

Aidha, Mwalimu alisema mkakati wa serikali ni
kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020 angalau wajawazito 80 kati ya 100
waweze kuhudhuria kiliniki angalau mara nne hivyo kutoa fursa ya
kufanyiwa vipimo mbalimbali ikiwamo malaria.

Kwa upande wake
mratibu wa ugonjwa wa malaria mkoa wa Dodoma, Fransis Bujiku amesema
kuwa Mkoa huo umefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria
kutoka asilimia 1 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 0.6 kwa sasa.
Bujiku amesema kuwa kwa pamoja wamefanikiwa kwa kutuna mazingira ikiwa
ni pamoja na kunyunyiza dawa ya kuua mbu kipindi cha masika na kufukia
madimbwi yote yanayotuamisha maji pamoja na kuwahamasisha wananchi
kulala kwenye vyandarua.

Siku ya malaria duniani inafanyika
kesho ambapo kitaifa itafanyikia mkoani Lindi ikiwa na kauli mbiu
isemayo Ziro malaria inaanza na mimi .
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akiwapongeza baadhi ya wanaume ambao waliwaleta watoto klinik wakati wa
kugawa vyandarua kwa wajawazito na watoto chini ya mwaka mmoja na nusu
katika hospitali ya Wilaya iliyopo Makole jijini Dodoma.

Share.

About Author

Leave A Reply