Tuesday, March 19

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA MRADI WA VIOSKI TEMBEZI JIJINI DODOMA

0Saturday, December 08, 2018

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amezindua
mradi wa vioski tembezi wa kampuni ya Sigara Tanzania (TCC).

Akizungumza
leo Disemba 8, 2018 Waziri Mhagama amesema kuwa mradi huo utasaidia
wajasiriamali wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo kuweza kujiajiri na
kupata kipato kitakacho wanufaisha kiuchumi.“Hii ni faraja kubwa kwetu
kama Serikali kuona mnaunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua
changamoto za ajira nchini kwa kuwawezesha wajasiriamali kuchangamkia
fursa za kujiendeleza kibiashara”, alisema Mhagama.

Aliongeza
kuwa Serikali inatambua mchango wa wadau na kuwataka wawekezaji wengine
waweze kubuni miradi kama hiyo yenye manufaa kwa wananchi.Aidha, Mhe.
Mhagama aliipongeza kampuni ya Sigara Tanzania kwa ubunifu na kuwasihi
waendelee kufanya vizuri katika nyanja nyingine kwa manufaa ya
watanzania kwa ujumla.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,
Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa ni jambo la faraja mradi huo
umezinduliwa Jijini Dodoma ikiwa ni fursa kubwa kwa wajasiriamali kuweza
kunufaika kiuchumi.

Naye, Mkurugenzi wa Masoko, Bi. Awaichi
Mawalla amesema kuwa Vioski 400 vitagawiwa nchi nzima kwa wajasiriamali
wadogo ambao wamekuwa wakifanya kazi na kampuni ya TCC na wataweza kuuza
bidhaa mbalimbali.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo wa vioski wa kampuni ya Sigara Tanzania (TCC). (Kushoto) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa pamoja na Naibu Waziri Mhe. Anthony Mavunde (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) wakimsikiliza Fundi Mkuu wa Vifaa Saidizi kwa Watu wenye Ulemavu Bw. Mwita Marwa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa Viungo Dodoma, Bw. Hassan Hussein.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali walioweza kunufaika na mradi huo, mara baada ya uzinduzi wa hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma, Disemba 8, 2018.

Share.

About Author

Leave A Reply