Wednesday, August 21

Watoto Wa Kike Zaidi Ya 2,454 Wapewa Mimba

0


Na, Editha Edward-Tabora 

Zaidi ya Watoto 2,454 wenye umri wa chini ya Miaka 20 katika Halmashauri ya Wilaya  Nzega Mkoani Tabora Watoto hao wanapata mimba za utotoni kwa takwimu za Mwaka 2018 Huku robo yao mwezi wa kwanza hadi wa tatu 2019 mimba chini ya miaka 20 zilikuwa 603 Huku Sababu zikielezwa 

Kuwa ni umasikini pamoja na ukatili wa kijinsia 

Takwimu hizo zimetolewa katika kikao kilichokutanisha wadau mbalimbali mjini Nzega  na shirika lisilo la Kiserikali la World Vision linaloendesha kampeni hii ya kupambana na Mimba na ndoa za utotoni likishirikiana  na Serikali ili kutokomeza janga hili ambalo linakwamisha ndoto za Watoto wa kike 

Bertha Mtesigwa ambaye ni Mratibu wa shirika la world Vision amesema Mradi huo una miaka saba ukitekelezwa na shirika hilo Lakini tatizo hilo linendelea kupungua japo amesema chngamoto haziishi 

“Mimba hizi zimechangiwa na Sababu mbalimbali ikiwemo ya kwanza ni umasikini uliokithiri kutoka katika jamii zetu za watu wa Nzega Lakini kumekuwa na uelewa mdogo kuhusu suala la Malezi Makuzi ya mtoto na mila potofu ambazo zimechangia sana kuongezeka kwa mimba za utotoni “Amesema Mtesigwa

Meneja wa shirika la world Vision John Masenza amesema vyombo vya dola vinaendelea kupambana na tatizo hilo na amewaomba Wananchi Kushirikiana na shirika hilo ili kukomesha mimba za utotoni 

Aidha idadi kubwa ya wanaopata mimba za utotoni ni wanafunzi wa shule za Msingi na shule za Sekondari.

 Wadau mbalimbali wakiwa katika kikao kilichoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la world Vision linalopambana na mimba za utotoni.

John Masenza meneja wa shirika la world Vision akizungumza na wadau.

Share.

About Author

Leave A Reply