Tuesday, March 19

Wateja wa Tigo Kanda ya Ziwa kufanya malipo kwa kutumia Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG)

0


Wateja
wa Kampuni ya Tigo wa mikoa ya Kanda Ziwa sasa wanaweza kufanya malipo
kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya
kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini kwenye App yake ya Tigo
Pesa. 

Akiongea
katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika jijini Mwanza, Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza
(MWAUWASA) Mecky Manyama alisema mfumo wa GePG umerahisisha upatikanaji
wa ankara na kufanya malipo kwa wananchi na kuongeza kuwa umeleta faida
nyingi ikiwa ni pamoja na kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa
taarifa, kupunguza ubadhirifu na kuongeza mapato kwa idara mbali mbali
na taasisi za Serikali 

“Mfumo
wa GePG, pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na
kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama
Tigo. Wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na
mashirika ya Serikali ikiwa ni pamoja na za kutoka MWAUWASA. Malipo pia
yanaweza kufanyika kwa njia mbali mbali za kimtandao, na kufurahisi na
mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya
mtandao.,” alisema Manyama 

“Kufanya
kazi kwa karibu na Serikali ili kufikisha huduma za kifedha kwa
wananchi wengi ni moja kati ya malengo mkakati yetu,” alisema Mkurugenzi
wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthuman Madatti 

Aliongeza
“Zaidi ya wateja milioni 7 wanaotumia huduma yetu ya Tigo Pesa sasa
wana uwezo zaidi wa kufanya malipo kwa haraka kwenda kwa taasisi, Wizara
na wakala wa Serikali zaidi ya 300 kupitia Tigo Pesa USSD, Tigo Pesa
App na QR Code,” 

Baadhi
ya taasisi za Serikali ambazo malipo yanaweza kufanywa kwa Tigo Pesa ni
pamoja na Wizara ya Ardhi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka za Miji, Mamlaka ya Bandari Tanzania
(TPA), Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Wizara ya Ardhi na
Maendeleo ya Makazi, Mamlaka ya Misitu (TFS), Wizara ya Utalii, Bodi ya
Utalii, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka za Maji katika miji ya Mwanza
(MWAUWASA), Tanga (Tanga UWASA), Dar es Salaam (DAWASA), Dodoma
(DUWASA), Hospitali mbali mbali kama vile Muhimbili, Mwananyamala na
idara nyingine zaidi ya 300. 

Ili
kufanya malipo kwa kutumia Tigo Pesa App na QR Code, wateja wa Tigo
wanahitaji kupakua App ya Tigo Pesa na kuscan QR code kisha kuingiza
namba ya siri ili kufanikisha muamala. 

Mkurugenzi
wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti (kushoto), akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa
Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG)uliofanyika jijini Mwanza leo.
Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama (kulia), akionyesha namna ya kutumia simu ya kiganjani kufanya malipo, wakati wa uzinduzi wa  Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG), ambao utatumika kufanya malipo kwa taasisi zaidi ya 300 za Serikali kwa kutumia mtandao wa Tigo. Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti.

Mkurugenzi
wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti (kulia), akionyesha kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) namna ambavyo simu ya kiganjani
kupitia mtandao wa Tigo inaweza kutumika kulipa malipo mbali mbali kwa
taasisi zaidi ya 300 za serikali wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa
Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG)uliofanyika jijini Mwanza leo.
Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo Ally
Maswanya

Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama (kulia), akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) , wakati wa uzinduzi wa  Mfumo wa Kielektronic wa
malipo ya serikali (GePG), ambao utatumika kufanya malipo kwa taasisi
zaidi ya 300 za Serikali kwa kutumia mtandao wa Tigo.Anayefuatia ni
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti na Mkuu wa Kitengo cha
Biashara na Serikali wa Tigo Ally Maswanya. 

Share.

About Author

Leave A Reply