Thursday, August 22

VITUO MAALUM VYA UCHENJUAJI KUJENGWA KATIKA MAENEO YA WACHIMBAJI WADOGO NCHINI

0


Na Zuena Msuya, Geita.

Serikali  inadhamiria kujenga vituo maalum vya uchenjuaji na kuvizungushia ukuta katika kila eneo lenye wachimbaji wadogo ili kudhibiti wizi na uuzwaji holela wa madini ya dhahabu katika maeneo hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila alisema hayo Februari 20, 2017 mkoani Geita ,wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Mfano na Mafunzo kwa wachimbaji wadogo kinachojengwa katika eneo la Rwamgasa mkoani humo.

Prof. Msanjila alisema kuwa vituo hivyo vitakapojengwa vitarahisisha ukusanyaji wa mapato na kuwasaidia wachimbaji kuuza dhahabu yao kwa bei halisi na kudhibiti walanguzi katika maeneo ya wachimbaji.
Vilevile alifafanua kuwa utaratibu unaotumiwa na wachimbaji wadogo hivi sasa kuchenjua dhahabu, umekuwa ukipoteza dhahabu nyingi ikilinganishwa na utumiaji wa njia za kisasa: Pia hakuna kumbukumbu sahihi na taarifa zilizo wazi zinazoonyesha soko halisi la uuzaji wa dhahabu inayochimbwa na wachimbaji wadogo katika maeneo mbalimbali nchini.

“Tunawachimbaji wadogo wa dhahabu wengi sana nchini hii, na wanapochimba wanapata dhahabu lakini ukiwauliza wanauza wapi dhahabu yao hakuna majibu sahihi, pia ukiuliza bei kila mmoja anamajibu yake, na kwa mtindo huu wanaikosesha serikali mapato, hali hii haikubaliki lazima idhibitiwe” alisisitiza Msanjila.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila, akishuka chini ya mgodi uliojengwa katika Kituo cha Mfano na Mafunzo ili kujiridhisha na ujenzi huo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila( katikati) akiwa chini ya mgodi uliojengwa katika kituo cha Mfano na Mafunzo kilichopo Rwamgasa, mkoani Geita.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila,( tatu kulia) na maafisa kutoka wizara ya madini na serikali ya kijiji waakiwa juu ya sehemu ya mtambo wa uchenjuaji katika Kituo cha Mfano na Mafunzo ,wakifanya ukaguzi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, (tatu kushoto) na alipotembelea mgodi wa Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo mkoani Geita (GEREMA) Christopher Kadeo( tatu kulia).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPARead More

Share.

About Author

Comments are closed.