Wednesday, August 21

VIONGOZI TUACHE KUWAGAWA WANACHAMA – MNEC KAGERA

0


Anaadika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV – Bukoba.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Ndg. Willbroad Mutabuzi amewataka Viongozi waliopewa dhamana ndani ya CCM kutowagawa wanachama, na kuwakumbusha kuwa Vyeo ni dhamana, na kuacha migogoro isiyokuwa na tija ndani ya Chama.

Akizungumza na Viongozi wa CCM Mara baada ya kuwasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Bukoba Mjini,  mapema Mei 30, 2019 Ndg. Mutabuzi amesema katika kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu mwakani, Viongozi waliopo madarakani katika ngazi mbalimbali ndani ya CCM, Hawana budi kuheshimiana na kuvumiliana kwa kila hali pasipo kugawanyika na kuwagawa wanachama.

Ndg. Mutabuzi amewakumbusha Viongozi hao kuwa nafasi walizonazo ni za muda tu kwani yeyote anaweza kupewa au kuwekwa katika nafasi hiyo, hivyo si busara kugawa wanachama katika makundi kwani Chama ni cha Wanachama na sio Mali ya Mtu Binafsi, na kuwataka wale wote wanaotumia Vitisho kwa wanaowaongoza kuacha Mara moja.

Aidha kwa upande mwingine MNEC huyo Ndg. Mutabuzi ameishukuru Serikali ya Wilaya Chini ya Mkuu wa Wilaya Deodatus Kinawiro, jinsi inavyotoa ushirikiano, na kuomba ushirikiano huo baina ya Taasisi hiyo na Ofisi uendelee na isiwe ni ushirikiano wa mtu na Mtu.

Mbali na shukrani hizo Ndg. Mutabuzi amewasisitiza Madiwani hasa wa CCM kutembea kifua mbele wakinadi Yale yote yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli, ikiwemo miradi ya Barabara, Umeme, Afya, Miundombinu  n.k ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Sambamba na Madiwani hao kurudi kwa wananchi kusikiliza na kuzitafutia Ufumbuzi kero zinazowakabili katika maeneo yao.

 Ndg. Mutabuzi akisaini katika Kitabu cha wageni Mara baada ya kuwasili Ofisi za CCM kabla ya kuongea na Viongozi wa Chama (W).

 Pichani ni MNEC wa Kagera Ndg. Willbroad Mutabuzi akivishwa Skafu na Vijana wa Chipukizi Mara baada ya kuwasili katika Ofisi za CCM (W) Bukoba Mjini.


Share.

About Author

Leave A Reply