Sunday, August 18

UJIO TAMASHA LA PASAKA MWANZA WAMFURAHISHA MBUNGE MABULA WA NYAMAGANA

0
*Awaomba wakazi Jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi,asema ni fursa kwa wanamuziki wa Injili

Na Ripota Wetu,Globu ya jamiii

MBUNGE wa Jimbo la Nyamagana ,Mwanza Stanslaus Mabula ameeleza kufurahishwa ha ujio wa Tamasha la Pasaka 2018 ambalo kwa mara ya kwanza linafanyika Jijini humo.

Ambapo amesema hiyo ni fursa kubwa kwa wasanii wa nyimbo za Injili katika Mkoa huo ambao una vipaji vingi vya waimbaji.

Akizungumza mapema leo na Michuzi Blog jijini Mwanza,Mabula amesema kutokana na ujio wa tamasha hilo, Kwaya nyingi za Jiji la Mwanza zitapata nafasi ya kuonesha uwezo na vipaji vyao vya uimbaji katika suala zima la kumtukuza Mungu kupitia nyimbo za Injili.

“Jiji la Mwanza lina vikundi/kwaya mbalimbali na mahiri katika uimbaji wa nyimbo za injili,hivyo tunaishukuru Kampuni ya Msama Poromotions,kutuletea tamasha la Pasaka litakalofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba April Mosi na baadae tamasha hilo litahamia kwa Wakazi wa Mkoa Simiyu ndani ya Mji wa Bariadi Aprili 2,2018,”ameeleza Mabula

Amesema tamasha la Sikukuu ya Pasaka pia litakuwa sehemu ya kuhamasisha utulivu,upendo na amani ya Tanzania ambayo Watanzania wengi wanaihitaji kuiona ikilindwa na kuimarika siku hadi siku.

Ametoa mwito kwa wakazi wa Jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo na kukongwa kwa nyoyo zao kupitia kwa waimbaji mbalimbali akiwemo Rose Muhando ambaye atazindua albamu yake itakayoitwa “USIFE MOYO”.

Wengine ni Upendo Nkone,Bone Mwaitege,Godluck Gozbert,Martha Baraka,Clement Paul,Beatrice Mwaipaja,Christina Shusho,Christopher Mwahangila,Jesca Honole na wengineo.

Mbunge wa Nyamagana,Mh.Stanslaus Mabula akifafanua jambo alipokuwa akizungumzia kuhusu ujio wa Tamasha la Pasaka 2018 kwa mara ya kwanza jijini Mwanza chini ya Kampuni ya Msama Promotions. Read More

Share.

About Author

Comments are closed.