Tuesday, March 19

UJENZI WA GATI NYAMISATI WAANZA, SHEHENA YA VIFAA YAANZA KUWASILI -KUANDIKWA

0


NA MWAMVUA MWINYI, KIBITI 


NAIBU
waziri wa Ujenzi, Elias Kuandikwa amesema ujenzi wa gati, uliokuwa
ukisubiriwa kwa kipindi kirefu na wakazi wa Nyamisati wilayani Kibiti
mkoani Pwani umeanza ambapo shehena ya vifaa vya ujenzi vimeanza
kuwasili tayari kwa ajili ya kazi. 


Aidha
amewatoa wasiwasi wakazi wa Mafia kuhusu gati la Kilindoni ,kwamba
linatarajiwa kuboreshwa kwa kuondoa dosari ndogondogo zilizopo ili liwe
la kisasa. 


Akizungumza
na wananchi wakati alipotembelea eneo litakapojengwa gati hilo, katika
muendelezo wa ziara yake mkoani hapo, Kuandikwa alisema ujenzi utakuwa
wa miaka miwili kwa gharama ya sh. bilioni 14 .

Alimtaka ,
mkandarasi wa gati hilo kufanya kazi inayotakiwa kwa kuhakikisha, ujenzi
unakamilika kwa wakati ikiwezekana kuukamilisha kabla ya miezi 24.
Kuandikwa
alisema, ujenzi umeshaanza na mkataba ulisainiwa tarehe 24,octoba mwaka
huu, ombi lake ni kuona mkandarasi anamaliza kazi haraka.
“Fedha
zipo hatutaki kuona mkandarasi anasuasua, gati litasaidia kurahisisha
usafiri kwani ndio kiu ya wakazi wa Nyamisati na Mafia”
“Itakuwa
gati la kisasa na sasa tunakwenda kufanya maboresho katika gati la
Kilindoni wilayani Mafia ili kuwa na gati la uhakika ,kwa kuwa
itazingatia ubora, teknolojia mpya kwa lengo la magati haya yaweze
kudumu kwa miaka mingi “alisisitiza Kuandikwa. 


Pamoja
na hayo, alielezea ujenzi huo utakwenda pamoja na maboresho ya barabara
ya Bungu -Nyamisati itakayosaidia kurahisisha usafiri .
Akiwa
barabara ya barabara ya Mkuranga -Kisiju kiwango cha lami, yenye urefu
wa 1.8km alimpongeza meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani
Pwani, Yudas Msangi kwa kubana matumizi kwenye miradi na kuweza kutumia
katika miradi mingine. 


Msangi
alisema kwasasa wanaendelea na kazi za kufungua na kuboresha baadhi ya
barabara muhimu kuelekea katika miradi mikubwa mbalimbali.

Share.

About Author

Leave A Reply