Tuesday, August 20

UCHUNGUZI WAANZA KUBAINI WALIOMUUA KWA RISASI MWANAFUNZI CHUO CHA USAFIRISHAJI

0


*Wizara ya Mambo ya Ndani yaelezea kinachoendelea
*Rais Magufuli aagiza waliohusika wachukuliwe hatua 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imewahakikishia Watanzania kuwa uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Aqwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi utafanyika kwa haraka na weledi mkubwa na kufafanua waliohusika na kifo hicho kwa namna yoyote ile hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Imesema tukio la mwanafunzi huyo limewasikitisha Watanzania wote na Wizara hiyo imeanza kufanya uchunguzi ili kupata taarifa sahihi za tukio la kupigwa risasi mwanafunzi huyo na kwamba iwe kwa ofisa wa polisi au viongozi wa kisiasa wakithibitika kuhusika watachukuliwa hatua ili iwe fundisho kwa wengine kwani Serikali haipo tayari kuona raia hata mmona anapoteza maisha.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yusufu Masaun wakati anaelezea tukio la kifo  cha mwanafunzi Aqwilina aliyekuwa anasoma mwaka wa kwanza katika chuo hicho.
UCHUNGUZI WAANZA 
Akizungumzia hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa kutokana na mauaji ya mwanafunzio huo, Masaun amesema tayari vyombo vya ulinzi na usalama vimenza kuchunguza tukio hilo ili kubaini waliohusika na kwa sasa ni mapema kusema fulani ndio amehusika moja kwa moja.

Amesema Serikali imesikitishwa na kifo hicho lakini uchunguzi unaendelea na atakayebainika kuhusika kwa namna yoyote hatua za kisheria zitachukuliwa.
“Tutahakikisha hatua zinachukuliwa haraka kwa waliohusika na hakuna ambaye ataachwa iwe ofisa wa polisi au viongozi wa vyama vya siasa.Kiujumla matatizo ya uvunjifu wa amani lazima yachukuliwe hatua na waliohusika kwenye hilo nalo lazima wachukuliwe hatua kali,”amesema Masauni.
Amefafanua wapo viongozi wa kisiasa ambao walikuwa wanatoa kauli za kuashiria uvunjifu wa amani ambao nao lazima wachunguzwe.
Amesema lengo la uchunguzi huo ni kupata taarifa sahihi ili asije kuoonekana hatua zimechukuliwa bila kufanyika uchunguzi, hivyo wameanza na uchunguzi ambao anaamini utakamilika kwa haraka.
Ameongeza uchunguzi huo utafanyika kwa weledi na umakini wa hali ya juu ili kuhakikisha haki inatendeka huku akieleza kwa sasa hawawezi kusema wamekamatwa watu wangapi kutokana na tukio hilo  ila uchunguzi ukikamilika watatoa taarifa kwa umma hatua zinazofuata.
Waziri wa Mambo ya Ndani Nchi, Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa abari mapema leo mchana jijin Dar,kuhusu kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Aqwilina Akwiline aliyeuawa kwa kupigwa risasi Mkwajuni,Kinondoni jijini Dar.Masauni amewahakikishia Watanzania kuwa uchunguzi wa kifo utafanyika kwa haraka na weledi mkubwa na kufafanua waliohusika na kifo hicho kwa namna yoyote ile hatua kali za kisheria zitachukuliwa. Picha Michuzi Jr.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPARead More

Share.

About Author

Comments are closed.