Tuesday, July 23

TANZIA: Advocate Martin Depores Matunda afariki dunia, kuagwa Jumatano Dar es salaam, kuzikwa kwao Bukoba Ijumaa

0


Ndugu yetu Martin amefariki ghafla Leo asubuhi nyumbani kwake Sinza jijini Dar es salaam.

Mipango ya mazishi ni ni kwamba mwili umepangwa kuagwa siku ya Jumatano saa NNE asubuhi nyumbani kwake Sinza Lion. Kufika msibani unafuata barabara moja kwa moja kupita Lion hotel,  mbele kule utakuta magari jirani na kanisa Katoliki lililo jirani na Lion Hotel. Baada ya kuagwa mwili utasafirishwa siku hiyo hiyo saa saba mchana utasafirishwa kwenda Bukoba kwa ajili ya mazishi ambayo yamepangwa kufanyika siku ya Ijumaa.


Globu ya Jamii inaungana na ndugu, marafiki na majirani katika msiba huu mzito kwa tasnia ya sheria. Mola na ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi – AMINA

Share.

About Author

Leave A Reply