Friday, May 24

STARS KUANZA NA SENEGAL AFCON.

0


Na Agness Francis, Michuzi Tv

UONGOZI wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) umetangaza rasmi gharama za tiketi za kutazama mechi za Fainali ya Africa (AFCON) inayotarajia kuanza juni mwaka huu zitakazofanyika  nchini Misri.

Ambapo shirikisho hilo limetangaza gharama hizo kwa madaraja mbalimbali.

Kwenye michezo ya hatua ya makundi ambayo itahusisha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” tiketi za daraja la 1 ni dola za kimarekani 29,tiketi za daraja la 2  ni 18 na tiketi za daraja la 3  kwa dola za kimarekani 6.

Hatua hiyo (Taifa Stars)  itacheza michezo mitatu ambapo itaanza dhidi ya Senegal ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Kenya na kumalizia hatua hiyo kwa kucheza na Algeria. 

Hatua ya robo fainali kwa gharama ya tiketi daraja 1 kwa dola za kimarekani  35  kwa daraja la 2 ni 24 na  la 3  ni 12, ikiwa hatua ya nusu fainali dalaja  la 1 ni  dola 59, la 2 ni 29 na la 3  kwa dola  18.

Wakati mchezo wa mshindi wa 3  itakua   daraja la 1 kwa dola 24 za kimarekani,  la 2 na la 3 kwa  12,ambapo  kwa mchezo wa fainali daraja la 1 n dola 106,la 2 44, na  la 3 ni 24.

Aidha Afisa habari na mawasiano TFF Cliffold Ndimbo amesema kuwa kwa yeyote mwenye nia ya kununua tiketi hizo za AFCON awasiliane na TFF mapema kabla ya kufungwa kwa muda wa maombi hayo. 

Share.

About Author

Leave A Reply