Monday, August 26

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN ASHIRIKI KATIKA MAZIKO YA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA ZFA MAREHEMU ALI FEREJ TAMIM KATIKA MAKABURI YA MWANAKWEREKWE ZANZIBAR

0


RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka
mchanga katika kaburi la Mareheme Ali Ferej, aliyekuwa Mwenyekiti wa ZFA
yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar leo 19-5-2019

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi na Wanamichezo katika maziko ya Marehemu Ali Ferej Tamim , aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Zanzibar(ZFA) yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akitowa
mkono wa Pole kwa Watoto wa Mareheme Ali Ferej Tamim, baada ya
kumalizika maziko hayo yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe
Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapijnduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,
akiwafariji na kutowa mkono wa Pole kwa Familia ya Marehemu Ramadhan
Abdalla Shaban, alipofika nyumbani kwa Kijiji cha Uzini Wilaya ya Kati
Unguja leo 19-5-2019

RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwafariji
na kutowa mkono wa Pole kwa Wajane wa Marehemu Ramadhan Abdalla Shaban,
aliofika Kijiji kwao Uzini leo kutowa mkono wa pole kwa familia

RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia
dua ikisomwa na Katibu wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil
Soraga alipofi kutowa mkono wa pole na kuifariji familia ya Marehemu
Ramadhan Abdalla Shaban , kijiji kwa Uzini Wilaya ya Kati Unguja leo
19-5-2019.(Picha na Ikulu)

Share.

About Author

Leave A Reply