Sunday, May 26

Rais Magufuli afanya kikao cha kazi na RC, RAS, DC, DAS na DED wote

0


Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Magufuli amewataka Wakuu wa
Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na
Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kujenga
ushirikiano na uhusiano mzuri baina yao ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu
yao.

Mhe.
Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo leo tarehe 16 Mei, 2019 katika kikao cha
kazi kati yake na viongozi hao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, na
kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa Majaliwa, baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu.
Mhe.
Rais Magufuli amewaonya baadhi ya viongozi hao ambao wamekuwa na migogoro baina
yao na hivyo kuathiri utendaji kazi na amesema endapo vitendo hivyo vitaendelea
hatasita kuchukua hatua ikiwa ni pamoja kuwaondoa katika nyadhifa zao.
Pamoja
na kuwataka kuwa waadilifu na wenye nidhamu kazini, Mhe. Rais Magufuli
amewataka kusimamia kwa ukaribu miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika
maeneo yao, kusimamia ukusanyaji wa mapato yote ya Serikali, kusimamia ulinzi
na usalama na kusimamia rasimali za umma.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza viongozi hao kwa kazi nzuri wanazozifanya zinazowezesha
mipango na mikakati mbalimbali ya Serikali kwenda vizuri na amewahakikishia
kuwa anawaamini na anatarajia wataendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa
majukumu yao.
“Ni matumaini
yangu baada ya kikao hiki cha leo sote tutakwenda kwa mwelekeo mzuri zaidi,
nendeni mkachape kazi, mimi ndiye niliyewaweka kwenye nafasi hizo na
ninafuatilia utendaji kazi wa kila mmoja wenu, sitarajii kusikia tena
hamuelewani miongoni mwenu”

amesisitiza
Mhe. Rais Magufuli.
Katika
kikao hicho Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero na changamoto mbalimbali ambazo
zinawakabili viongozi hao katika maeneo yao ya kazi na ameahidi kwenda kuzishughulikia.
Kabla
ya kuanza kwa kikao hicho, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Juma Zuberi
Homera kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Mhe.
Homera pia amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na
Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela.
Baada
ya kikao hicho, viongozi hao wamekula futari na Mhe. Rais Magufuli aliyoiandaa
kwa ajili yao.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Wakuu wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU 

Share.

About Author

Leave A Reply