Sunday, August 18

PASAKA YAWA CHUNGU SRI LANKA, MILIPUKO YAUWA MAMIA

0


 Makanisa na hoteli zashambuliwa, raia wa kigeni 35 wapoteza maisha.

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAKATI  Waumini wa Madhehebu ya kikristo ulimwenguni wakisherekea sikukuu ya Pasaka leo Machi 21, Wananchi wa Sri Lanka wameamshwa na milipuko mikubwa katika Makanisa na Hoteli jijini Colombo.

Katika mashambulio yapatayo matano watu 156 wamethibitika kupoteza maisha huku ikihofiwa kuwa idadi inaweza kuongezeka kutokana na majeruhi wengi kuwa katika hali mbaya. Mji mkuu wa nchi hiyo, Colombo kumetokea shambulio linaelezwa kupigwa katika hoteli iliyo karibu na  hifadhi kubwa ya wanyama nchini humo na polisi wameeleza kuwa watu wawili wamefariki dunia.

Aidha milipuko mitatu imetokea katika makanisa (katoliki) na milipuko mingine imetokea katika hoteli za kitalii za Cinnamon Grand, Kingsbury na Shangri -La- iliyopo katikati ya mji wa Colombo.

Mashambulio hayo yamesababisha majeruhi 400 waliokuwa wamekwenda kuabudu katika sikukuu ya Pasaka.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Aljazeera makanisa yaliyoshambuliwa ni pamoja na kanisa la Mtakatifu Anthony Shrine Colombo, kanisa la Mtakatifu Sebastian Negombo linalopatikana kilometa 30 kutoka mji mkuu pamoja na kanisa la Batticaloa lililopo kilometa 250 Mashariki kutoka Mji wa Colombo.

Waziri mkuu nchini humo Ranil Wickremesinghr ameitisha kikao cha dharura cha viongozi wa juu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini humo na kuelekeza kuwepo kwa kikao cha dharura cha Bunge mapema Jumatatu.

Msemaji wa polisi Ruwan Gunasekera amesema kuwa majeruhi wamekuwa wakiokolewa huku Polisi wakiendelea na uchunguzi.

Picha katika mitandao ya kijamii zilionyesha paa za makanisa hayo zikiwa zimeharibiwa kwa milipuko hiyo huku watu wakionekana wametapakaa damu.

Vilevile imeelezwa kuwa kati ya watu waliopoteza maisha watu 35 ni raia wa kigeni na bado washambuliaji hawajafahamika.

Katika kikao cha dharura kilichofanyika mapema baada ya tukio hilo waziri wa uchumi na masuala ya umma Harsha de Silva kupitia mtandao wa tweeter ameandika kuwa mashambulio mawili yametekelezwa nchini humo wengi wameathirika wakiwemo wageni na amewataka wananchi kuwa watulivu na kubaki majumbani.

Share.

About Author

Leave A Reply