Saturday, May 25

PANAFRICAN ENERGY TANZANIA YASAINI MKATABA WA KUFADHILI UJENZI MIRADI YA AFYA WILAYA YA KILWA

0


Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imesaini mkataba wa ujenzi wa Kituo cha Afya Somanga na upanuzi wa hospitali ya Wilaya Kinyonga.

Mkataba
huo wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia mbili
(1.2bilion) umesainiwa kati viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
na kampuni ya Pan African Energy ambao ni wadau wa maendeleo katika
Wilaya ya Kilwa. Utiaji saini huo umeshuhudiwa na wawakilishi wa kampuni
ya Pan African na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Ndg. Renatus Mchau ameishukuru kampuni
hiyo kwa msaada huo uliokuja kwa wakati na kueleza kuwa kwa muda mrefu
Wilaya ya kilwa ilikuwa na changamoto katika sekta ya Afya lakini kwa
sasa changamoto hizo zinakaribia kwisha kutokana na halamshauri yake
kuweka nguvu katika kuzitatu.


‘ Tangu mwaka 2017 tumepokea zaidi
ya shilingi bilioni moja na milioni mia nane kutoka ofisi ya Rais
TAMISEMI katika mpango wa uboreshaji wa Miundo mbinu ya sekta ya Afya
ambapo vituo vinne vya Afya vya Masoko, Tingi, Pande na Nanjilinji, na
sasa mchango wa hawa wadau wametuongezea nguvu nyingine katika
kuendeleza sekta ya Afya.


Alisema msaada huo wa Pan African
utaongeza idadi ya vituo vya Afya kutoka vitano vya sasa hadi sita
ambapo kati ya hivyo vituo vinne vitakuwa na uwezo wa kufanya upasuaji
na kuongeza damu kwa wanawake wajawazito.


Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe.Abuu Mjaka amewashukuru
kwa mara nyingine kampuni hiyo kwa msaada huo kwani ni mara ya pili
wanatoa msaada mkubwa baada ya ujenzi wa awali wa kituo cha Afya cha
Nangurukuru. ‘Nyie sasa tunawatambua rasmi si kama wadau tu bali familia
ya Kilwa’’ aliongeza Mhe.Mjaka.


Ujenzi Kituo cha Afya cha
Somanga ulianza kwa Mchango wa nguvu za wananchi ambapo mpaka sasa
jengo la mapokezi lipo katika hatua ya linta ambapo zaidi ya shilingi
milioni sabini kutokana na mchango wa wananchi , halmashauri pamoja
mchango binafsi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt.John Pombe
Magufuli wa shiingi milioni ishirini(20,000,000) aliyoitoa mwaka 2017
akiwa katika ziara mkoani Lindi. Mhe.Rais alitoa msaada huo baada ya
kuombwa na wananchi waliomsimamisha katika kata ya Somanga, msaada huo
ulikuwa chachu kwa wanachi wa kata hiyo na hivyo wakaanda kuchangia
nguvu zao.


Upanuzi huo utahusisha ujenzi wa Jengo la
mapokezi,Jengo la wazazi, Upasuaji , chumba cha kuhifadhia maiti na
chumba cha kufulia nguo vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya milioni
mia nane na thelathini.


Katika hospitali ya Wilaya ya Kinyonga
upanuzi utahusisha chumba cha kuhifadhia maiti na Bohari ya dawa thamani
ya shilingi milioni mia nne.


Baada ya kukamilika kwa ujenzi
Kituo cha Afya cha Somanga, Wilaya ya Kilwa itakuwa na vituo vya Afya
sita ambavyo ni Somanga, Tingi, Masoko,Nanjilinji , Pande na Njinjo.
.

Mwanasheria wa kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania Ritha Mohele na Meneja uwajibikaji kwa jamii wa Kampuni hiyo, Andrew Kashangaki, wakiwapa mkataba uliotiwa saini kwa ajili ya ufadhili wa ujenzi wa miradi ya afya itakayo gharimu zaidi ya billion moja za kitanzania.miradi hiyo sehemu ya kuhifadhia maiti, duka la dawa la wilaya na marekebisho ya hospital ya Somanga kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kilwa Abuu Mjaka na DED wa halmashauri ya wilaya hiyo Renatus Mchau.

Mwanasheria wa kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania, Ritha Mohele akisaini mkataba kwa niaba ya kampuni hiyo,kwa ajili ya ufadhili wa ujenzi wa miradi ya afya itakayo gharimu zaidi ya billion moja za kitanzania.miradi hiyo sehemu ya kuhifadhia maiti, duka la dawa la wilaya na marekebisho ya hospital ya Somanga.

Baadhi ya mashuhuda walio hudhuria kushuhudia mkataba uliotiwa saini kwa ajili ya ufadhili wa ujenzi wa miradi ya afya itakayo gharimu zaidi ya billion moja za kitanzania.miradi hiyo sehemu ya kuhifadhia maiti, duka la dawa la wilaya na marekebisho ya hospital ya Somanga kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya kilwa Abuu Mjaka,na DED wa halmashauri ya wilaya hiyo Renatus Mchau.

Share.

About Author

Leave A Reply