Saturday, August 24

NYOTA WA ZAMANI WA TAIFA STARS JELLAH MTAGWA YU HOI KITANDANI, ANAHITAJI MSAADA WAKO

0


Mchezaji kandanda wa zamani wa Taifa Stars na Yanga na Pan
African Jellah Mtagwa yupo kitandani akiugua kiharusi na anahitaji msaada wa
matibabu pamoja na kujikimu kimaisha.
Mtagwa, ambaye hivi sasa amepooza nusu ya mwili wake,
anaishi Manzese Friend’s Corner  jijini Dar es salaam pamoja na familia yake akiwa hana hili
wala lile kutokana na maradhi hayo na ufukara.
Wadau na mashabiki wa mpira wa miguu wameelezea masikitiko
yao kwa hali kama hiyo kumkumba aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya Taifa Stars
ambaye picha yake iliwekwa kwenye stempu kutokana na mchango wake uliotukuka
kwa nchi.
Wengi wanahoji endapo kama Shirika la Posta lilimlipa
mchezaji huyo mrabaha wa kuwekwa sura yake mwenye stempu, na kama Shirikisho la
Mpira nchini (TFF) wana taarifa zake na kama wanamsaidia kwa choche.
Hivi tunavoongea umoja wa wachezaji soka wa zamani  (UMSOTA) wameanzisha harambee ya kumsaidia mwenzao huyo kwa kuchangishana ili
kumsaidia.
Tayari umoja huo umetoa ombi la msaada kwa wasamaria wema
kumsaidi Jellah Mtagwa kwa kutangaza namba yake ya simu Namba 0755 693330 kwa
yeyote atakayeguswa.


 Baadhi ya wachezaji soka wa zamani wakiwa wamemtembelea Jellah Mtagwa nyumbani kwake Manzese Friend’s Corner jijini Dar es salaam kumjulia hali na kumpatia msaada

 Baadhi ya wachezaji soka wa zamani wakiwa wamemtembelea Jellah Mtagwa nyumbani kwake Manzese Friend’s Corner jijini Dar es salaam kumjulia hali na kumpatia msaada

 Baadhi ya wachezaji soka wa zamani wakiwa  na wanafamilia baada ya kumtembelea Jellah Mtagwa nyumbani kwake Manzese Friend’s Corner jijini Dar es salaam kumjulia hali na kumpatia msaada

Stempu iliyowekwa picha ya Jellah Mtagwa

Jellah Mtagwa akisimulia adha ya maradhi yake

Share.

About Author

Leave A Reply