Wednesday, August 21

NITABAKI KUWA MWANACHAMA MWADILIFU WA CHAMA CHA MAPINDUZI NA SERIKALI YAKE- Amos Makalla

0


Aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makala (kulia)  hii leo amekabidhi rasmi ofisi kwa mkuu wa mkoa mpya Mh Juma Homera aliyepewa nafasi hiyo baada ya Makalla kutenguliwa  nafasi ya ukuu wa mkoa huo na Rais Dkt John Magufuli hivi karibuni.

======  ======   ======== ======

– Asema Amekitumia Chama cha mapinduzi na Umoja wa vijana kwa Muda mrefu na  vipaji, uzoefu alionao atandelea kuwa Kada wa mstari wa Mbele  wa Chama cha Mapinduzi

– Amemshukuru Rais Dr John  Pombe Magufuli kwa kumuamini kwa nafasi ya Ukuu wa Mkoa kwa miaka 4

Amesema mwaka 2015 Alipokosa Ubunge ilitosha yeye kubaki mwananchi na mwana ccm tu huko Mvomero  Rais wa awamu ya 4  mhe Jakayla Kikwete alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na  Rais Dr John Magufuli alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya  na baadaye Katavi

– Amewashukuru wananchi na viongozi wa ngazi zote dini na serikali kwa kumpa ushirikiano katika Kipindi cha miezi 10 alipokuwa mkuu wa mkoa wa Katavi na Amewaomba wananchi na viongozi wampe ushirikiano wa kutosha mkuu wa mkoa Mpya Juma Homela

Share.

About Author

Leave A Reply