Tuesday, August 20

NEWS ALERT: PALAGYO APITA BILA KUPIGWA UBUNGE JIMBO ARUMERU MASHARIKI

0


Na Woinde Shizza wa Michuzi TV, Arusha 

Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi  (CCM) Bw. John Pallagyo (pichani) amepita bila kupigwa katika uchaguzi Mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki  baada ya wagombea wenzake 10 kushindwa kusimama kwa kukosa sifa . 

 Akizungumza wakati akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bw. Emmanuel Mkongo alisema kuwa jumla ya wagombea 11 walichukuwa fomu ya kugombea ubunge wa jumbo hilo na wagombea Tisa wamerejesha fomu hizo huku wagombea watatu wakiwa hawajarejesha kabisa 

Alisema kuwa wagombea hao Tisa wameshindwa kupitishwa katika kinyanganyiro hicho kutokana na kukosa sifa baada ya kushindwa kutimiza mashariti ya uchaguzi. 

 Baadhi ya wagombea hao ambao wameshidwa kukithi vigezo ni pamoja na wagombea watatu ambao hawakuteuliwa kwasababu hawajarudisha fomu, huku wengine wakiwa saba wakiwa wamerejesha lakini hawajakizi vigezo vikiwemo kutolipa dhamana ya kugombea ubunge ambayo inagharimu shilingi elfu 50, kukosa wadhamini pamoja na kutoleta hati ya kiapo kutoka kwa mwanasheria ama hakimu. 

 Alisema katika fomu hizo ni fomu moja tu (ya mgombea wa CCM) ndio ambayo ilikuwa haina mapungufu ya kisheria hivyo alitumia nafasi hiyo kumtangaza John Pallagyo kupita bila kupigwa na kuteuliwa kuwa mbunge mteule wa jimbo la Arumeru mashariki/

Akizungumza leo ofisi za halmashauri ya wilaya ya Meru, mara baada ya kutangazwa kuwa mbunge mteule kupitia chama cha mapinduzi, John Pallagyo  ameshukuru Sana kwa hatua hiyo na pia ameshukuru viongozi wa ngazi zote ambao walionyesha imani kwake na kuhakikisha jina linarudi kwenye kinyanganyiro hicho. 

 “Kitu cha kwanza nitakachofanya nipamoja na kuhakikisha Barabara zinatengenezwa kwani Jimbo hili halina barabara kabisa, sambamba na maji, pamoja na umeme kwani wananchi wa Jimbo hili wameteseka Kwa muda mrefu sasa. “alisema Pallagyo. 

 Aidha pia alisema kuwa kwa vile amepita kitu cha kwanza atakachomuomba Rais John Pombe Magufuli ni kutimiza ahadi yake ambayo aliwaahidi wananchi wa Meru kipindi alipopita kuomba kura mwaka 2015 ya kuwajengea barabara kilometa tano kwa kiwango cha lami. 

Share.

About Author

Leave A Reply