Monday, March 25

MWANAMKE APAMBANA NA JAMBAZI MWENYE SILAHA AKIMUOKOA MUMEWE,

0Mkazi wa Kijiji cha Mahyolo, Kata ya Nyamihyolo, Wilayani Bunda, Mkoa wa
Mara, Busimba Malegesi amemuokoa mumewe asiuawe na jambazi mwenye
silaha ambaye alivamia katika nyumba yao na kuanza kumshambulia mwanaume
huyo kwa kumkatakata mapanga mwili mzima.

Busimba alimrukia
jambazi huyo kiunoni na kumuangusha chini na kufanikiwa kumnyang’anya
panga pamoja na tochi ambazo alikua nayo wakati anamshambulia mumewe
aitwaye Samson Malegesi (62).

Tukio hilo la kusikitisha
lilitokea saa 7:30 usiku wa kuamkia Ijumaa wakati familia hiyo ikiwa
imelala ndipo jambazi huyo alivunja mlango na kuingia moja kwa moja
chumbani kwa wanandoa hao na kuwasha tochi kumsaka Malegesi na baada ya
kufanikiwa kumuona alianza kumshambulia kwa kumpiga mapanga kichwani,
mikononi, kwenye mbavu na kusababisha damu nyingi kumwagika.

Wakati
jambazi hilo akiendelea kumshambulia Malegesi, mkewe alikua naye
anapambana kwa kumzuia asimshambulie mumewe, lakini jambazi hilo
lilizidiwa baada ya mwanamke huyo kupata nguvu zaidi na kufanikiwa
kumuangusha chini na kuhakikisha silaha aliyoishika mkononi
akinyang’anywa kwa urahisi kutokana na kubanwa kwa juu na mwanamke huyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimwangalia mgonjwa ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Mahyolo, Wilayani Bunda, Samson Malegesi aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo, Busimba Malegesi (katikati), alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Mgonjwa huyo amelazwa katika Hospitali ya Kibara, Wilayani humo akiendelea kupewa matibabu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimwangalia mgonjwa ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Mahyolo, Wilayani Bunda, Samson Malegesi aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Kulia ni Muuguzi wa hospitali ya Kibara, Godliver Josephat, ambapo mhonjwa huyo amelazwa akipatiwa matibabu. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akiingia Hospitali ya Kibara Wilayani Bunda kumwangalia mgonjwa aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibara, Wilayani humo, Mkaguzi Boniface Mwalupale. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akiondoka Hospitali ya Kibara Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, mara baada ya kumwangalia mgonjwa aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibara, Wilayani humo, Mkaguzi Boniface Mwalupale.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Share.

About Author

Leave A Reply