Sunday, August 25

Muhimbili yafanya usafi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar

0


Timu ya  Michezo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  leo imeshiriki kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya  Hospitali ya Mnazi  Mmoja Zanzibar kwa lengo la kudumisha uhusiano  na ushirikiano kati ya hospitali hizi.

Ushirikiano huu unadumisha utamuduni wa hospitali hizi kutembeleana kila mwaka na kushiriki  michezo ya Pasaka ambayo imeanza leo Kisiwani Zanzibar.

 Mkurugenzi wa Idara ya Tiba kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt.Juma Mbwana  amesema ushirikiano baina ya hospitali hizi ni mzuri na pia wamefurahi kujumuika pamoja katika kufanya   usafi. 

Mkurugenzi huyo amesema na kuahidi shughuli ya usafi itakuwa ikifanyika mara kwa mara ili kudumisha uhusiano zaidi.

“Serikali ya Mapunduzi Zanzibar chini ya Rais Dkt. Mohamed Shein na Wizara ya Afya tumefurahiswa na ugeni huu kwani michezo ni afya, pia kuja kwenu hapa hospitalini kufanya usafi   kumewafariji na  kuhamasisha wananchi kufanya usafi,” amesema Dkt. Mbwana.

Kwa upande wake   Mkuu wa msafara  wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Praxeda Ogweyo amesema katika sekta ya afya michezo na usafi ni vitu muhimu na kwamba lazima mambo haya yatekelezwe.

Pia, ametoa wito kwa jamii  kushiriki kwa hiari kutoa huduma za usafi hospitalini.

“sisi tumetokea kwenye sekta ya afya tumeona ni vizuri tutumie fursa hii kujumuika na wenzetu katika sekta ya afya katika michezo, lakini tumeona tuje tufanye usafi hospitali kwa kuwa usafi ni muhimu kwenye sekta ya afya,” amesema Dkt. Praxeda.

Michezo hii ya Pasaka  hufanyika kila mwaka zikihirikisha timu ya Muhimbili na Wizara ya Afya Zanzibar.

 Mkurugenzi wa  idara ya tiba kutoka wizara ya afya Zanzibar Dkt. Juma S. Mbwana, akizungumza jambo kwa wanamichezo wakati wa zoezi la usafi ambapo wameshiriki katika kufanya maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.

 Mkurugenzi wa huduma za tiba shirikishi kutoka Hospitali yaTaifa Muhimbili Dkt. Praxeda Ogwayo (kulia) akishiriki kufanya usafi katika  moja ya wodi hospitali hapo, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa huduma za uuguzi na ukunga Bw. Yassin Mungwatosha kutoka muhimbili.

 Baadhi ya wanamichezo wa Muhimbili wakishiriki zoezi la usafi katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Wanamichezo wa Muhimbili wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi.

Share.

About Author

Leave A Reply