Thursday, July 18

MKUU WA MKOA WA MBEYA AKABIDHI MAGARI MAWILI NA PIKIPIKI NNE KWA JESHI LA POLISI MBEYA.

0


Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amefanya ziara ya kikazi tarehe 30.11.2018 kwa kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwake.

Katika ziara hiyo, Mhe.Chalamila alikabidhi magari mawili aina ya Probox kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya ili yatumike katika kuimarisha doria katika barabara kuu ili kupunguza ajali na kupambana na uhalifu.

Aidha Mhe.Chalamila alikabidhi pikipiki nne aina ya FEKON zilizotolewa na mdau wa Jeshi la Polisi kwa askari Polisi walioonyesha uaminifu katika kazi kwa kukamata fedha zaidi ya Tshs.Milioni 17 zilizokuwa zimeibwa dukani kwa mfanyabiashara mmoja huko Wilayani Chunya.

Sambamba hilo, Mhe.Mkuu wa Mkoa amekagua kambi ya Polisi Mbeya na kuahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha unafanyika ujenzi wa nyumba za kisasa za kuishi askari ili kuongeza morali ya kiutendaji kwa askari wa Jeshi la Polisi.

Mhe.Mkuu wa Mkoa alikamilisha ziara yake ya kikazi kwa kuzungumza na askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na kusisitiza uadilifu, nidhamu na uaminifu. Aidha amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kudhibiti ajali za barabarani hasa madereva wa Pikipiki @ bodaboda ambao hawataki kutii sheria za usalama barabarani.

Pia Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alitumia ziara hii kutoa tamko kwa wakazi wa Mbeya kuwa siku ya tarehe 09.12.2018 [uhuru wa Tanganyika] watumishi wote wa umma watashiriki kazi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa majengo ya umma, kufyetua tofali, kuchota maji kwa ajili ya ujenzi na kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yote ya Mkoa wa Mbeya.

 Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akiwasili kuanza  ziara ya kikazi

  Pikipiki nne aina ya FEKON zilizotolewa na mdau wa Jeshi la Polisi kwa askari Polisi walioonyesha uaminifu katika kazi kwa kukamata fedha zaidi ya Tshs.Milioni 17 zilizokuwa zimeibwa dukani kwa mfanyabiashara mmoja huko Wilayani Chunya.

  Magari mawili aina ya Probox kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya ili yatumike katika kuimarisha doria katika barabara kuu ili kupunguza ajali na kupambana na uhalifu.

 Mhe.Chalamila akikabidhi magari mawili aina ya Probox kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya

Mhe.Mkuu wa Mkoa akikagua kambi ya Polisi Mbeya na kuahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha unafanyika ujenzi wa nyumba za kisasa za kuishi askari

Share.

About Author

Leave A Reply