Friday, July 19

MEYA MWITA AKUTANA NA UJUMBE WA WATU WENYE UALIBINO

0


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MEYA 
wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amekutana na kufanya mazungumzo na
ujumbe wa Shirika la kutetea haki na ustawi wa watu wenye ualbino la
Under The Same Sun, tawi la Tanzania.

Katika mazungumzo hayo
yaliyofanyika jana shirika hilo lililowakilishwa na Ofisa Uraghibishaji
Kondo Seif, limeomba fursa ya kukutana na  madiwani wa Mkoa wa Dar es
salaam wanapokuwa kwenye vikao vya kazi, ili kuwaeleza masuala
mbalimbali yanayohusu dhana nzima ya ualbino na changamoto zake.

Taarifa ya Ofisa Habari wa Ofisi ya Meya Christina wa Jiji la Dar es Salaam Christina amesema Mwagala Meya wa jiji
Meya
Mwita aliridhia ombi la shirika la Under The Same Sun na kuahidi ofisi
yake kusaidia kwenye jitihada za kumaliza madhila wanayoyapata watu
wenye ualbino.

Itakumbukwa katika miaka ya 2006, Tanzania
iligubikwa na habari za matukio ya mauaji na ukataji wa viungo vya watu
wenye ualbino, na kutumia viungo vya miili ya watu hao  kwa imani za
kishirikina, kwa kuamini kuwa watafanikiwa kwenye shughuli zao za
kiuchumi.

Tangu wakati huo, shirika la Under The Same Sun
limekuwa likizunguka maeneo mbalimbali nchini kutoa elimu kuhusu
ualbino, jinsi unavyopatikana sambamba na kutoa ufadhili wa kielimu kwa
watu wenye ualbino, ambapo zaidi ya wanafunzi 400 nchi nzima wanafaika
kwa kulipiwa gharama za elimu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi hadi vyuo
vikuu.

 Afisa uraghibishaji wa shirika la Under the Same Sun, Kondo Seifu akimuonesha  Mstahiki Meya Isaya Mwita picha mbalimbali zilizomo kwenye kitabu hicho  jumbe mbalimbali zinazo elezea walemavu hao

 Afisa uraghibishaji wa shirika la Under the Same Sun, Kondo Seifu
akizungumza jambo na Mstahiki Meya Isaya Mwita jumbe mbalimbali zinazo elezea
walemavu hao

 Afisa uraghibishaji wa shirika la Under the Same Sun, Kondo Seifu
akimkabidhi Mstahiki Meya Isaya Mwita jumbe mbalimbali zinazo elezea
walemavu hao

Share.

About Author

Leave A Reply