Friday, April 19

MAAFISA NA WASHIRIKI WA KOZI WA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA (NDC) WAFANYA ZIARA

0


 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike
(kushoto) akisalimiana na Mkufunzi Mkuu Kanali Erick E. Mhor (kulia). Wa pili
toka kushoto ni Mkalimani toka Jeshi la China, Brig. Jenerali Liang Hongshan na
wapili toka kulia ni Brig. Jenerali M.N.Mkeremy.

 Mkuu wa Msafara Commodore Mumanga (kushoto) akimkabidhi Naibu Kamishna wa Magereza John Masunga,  zawadi maalum ya Mkuu wa Jeshi hilo.

 . Insp. Mwasimba Boge wa Jeshi la Magereza (wa
pili kulia) akitoa maelezo ya baadhi ya nguo zinazoshonwa na wafungwa kama njia
mojawapo ya Urekebishaji ndani ya Kiwanda cha Ukonga.

 Mkuu wa msafara wa Maafisa na washirirki wa kozi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) Commodore (Brig. Jenerali-Navy) M.M.Mumanga (kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Viwanda Vidogo Vidogo wa Jeshi la Magereza Naibu Kamishna John Masunga. Kulia ni Naibu Kamishna Jeremiah Katungu.

 Mkuu wa msafara Commodore Mumanga(kushoto) akitoa neon la shukrani kwa Kamishna Jenerali wa Magereza (hayupo pichani). Kulia ni Brig. Jenerali Zhang Yongxi ambaye ni Mkufunzi Mkuu toka Jeshi la China.

 Askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia
Magerezani (KMKGM) wakiwaonesha wakufunzi na wanafunzi toka Chuo cha Ulinzi cha
Taifa jinsi ya kukabiliana na wahalifu wakorofi.

Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali
Phaustine Kasike (wan ne toka kushoto, walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja
na Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Magereza, Viongozi Waandamizi wa Chuo cha
Ulinzi cha Taifa pamoja na wanafunzi wa Chuo hicho.
Share.

About Author

Leave A Reply