Monday, March 25

Halotel, Biko kunogesha michezo msimu wa sikukuu.

0


      Na.Khadija seif,globu ya jamii

KAMPUNI ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel nchini  imeingia katika makubaliano rasmi na kampuni ya michezo ya kubahatisha na kubashiri ya Biko ili kuongeza msisimko na ushiriki kwa wadau wa michezo hiyo nchini katika msimu wa huu sikukuu.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Ofisi za Halotel Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Halotel Mhina Semwenda amesema ushirikiano huu baina ya Kampuni ya Halotel na Biko utawezesha wateja wetu kuweza kushiriki na kupata fursa ya kujishindia fedha zitazowawezesha kujiongezea kipato na hivyo kuboresha maisha yao.

Pia ameeleza kuwa hii ni fursa kwa wateja  wote wa Halotel mijini na vijiini kuweza kushiriki katika michezo ya kubahatisha na kubashiri kama vile mpira wa miguu , mpira wa kikao,rugby,cricket,Tennis na mingineyo ambapo hapo kabla hawakuweza kupata fursa kushiriki katika michezo hiyo.

Kwa upande wake Meneja Masoko Biko Goodhope Heaven  amefafanua kuwa Biko ni kampuni kubwa na madhubuti inayojihusisha na michezo ya kubahatisha kwa kufanya miamala Kwenye simu za Mkononi.

Aidha heaven ameeleza ushirikiano huo utawezesha wateja wanaotumia mtandao wa Halotel kupitia huduma ya kifedha ya Halopesa kupata fursa ya kuvuna mamilioni kutoka Biko kwa kubahatisha na pia kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali na Bikosports.

Biko inaendelea kusisitiza wabashiri kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea na mpaka sasa watu waliobashiri na kubahatika kushinda wameneemeka kwa kutokana na kushinda zawadi za fedha,pikipiki na nyuma aliongezea  heaven.

 Mkuu wa
mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda
  akizungumza
na waandishi wa Habari jinsi mteja wa Halopesa anavyoweza kujiunga na kushiriki
katika michezo ya kubashiri inayoendeshwa na kampuni ya Biko. Pamoja nae kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven (kulia) na Mkuu wa Biashara wa Halopesa
Magesa Wandwi.

Meneja Masoko
wa Biko Goodhope Heaven, akizunguzumza na  waandishi wa Habari  jinsi mteja wa Halotel  anavyoweza kushiriki mchezo wa bahati nasibu
ya biko na kupata nafasi ya kushinda Nyumba na Mamilioni ya Biko katika msimu
huu wa sikukuu (kulia) ni Mkuu wa mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda (kushoto).

Share.

About Author

Leave A Reply