Saturday, August 24

CHUO KIKUU HARVARD WAMTUNUKU SHAHADA YA UDAKTARI WA HESHIMA ANGELA MERKEL

0


Na Ripota,Kimataifa 

KANLESA wa nchini Ujerumani Angela Merkel ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima ya Chuo Kikuu maarufu cha Harvard. 

Rais wa Chuo cha Havard Larry Bacow ambaye ndiye aliyemtunukia Merkel tuzo hiyo amesema kuwa Kansela huyo wa Ujerumani ni mwanasiasa mwenye nguvu barani Ulaya. 

Wakati wa sherehe za kutunukiwa kwa Shahada hiyo ya Udaktari, chuo hicho kimemsifu Merkel kwa matamshi yake “Tutaweza kulisimamia hili” wakati wa mgogoro wa wakimbizi ulioanza mwaka 2015 nchini Ujerumani wakati aliporuhusu idadi kubwa ya wakimbizi na kukabiliwa na ukosoaji mkubwa nchini mwake. 

Akizungumza kwenye hotuba yake kwa wanafunzi, wakati wa mahafali ya 368 ya chuo hicho cha Havard, Merkel amewaonya wanafunzi dhidi ya kuchanganyikiwa na kuuchukulia uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa ni uongo. 

CHANZO- DW

Share.

About Author

Leave A Reply