Sunday, August 25

Benki ya NMB Yazidi kujitanua, yazindua Rasmi Tawi lake Mbogwe

0


Benki
ya NMB imezindua tawi jipya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kwa lengo la
kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha kwa wateja hivyo kusaidia ukuaji
wa uchumi katika kanda ya Magharibi. Hilo ni tawi la 25 kwa mkoani Geita
na la 229 nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa hafla ya
kuzindua tawi hilo, mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Geita Eng. Gabriel
Luhumba amesema ufunguzi wa tawi hilo umekuja wakati muafaka kwa kuwa
ofisi za serikali zinampango wa uchumi wakimkakati ambao utafanya Geita
kuwa chachu ya maendeleo nchini.

Akiongea na wananchi wa wilaya
ya Mbogwe Eng. Gabriel Luhumba pia ametoa rai kwa wananchi kubadilika
na kuacha mazoea ya kuweka pesa majumbani na kuwataka kuwa na tabia ya
kuweka benki na kwenye taasisi za fedha.

Eng.Luhumba alisema
wananchi wa mkoa wa Geita wenye neema nyingi ya madini aina ya dhahabu
wamekuwa na tabia ya kutunza fedha zao nyumbani hali ambayo imekuwa ni
hatari kwa usalama wa maisha yao na kuwataka kuacha tabia hiyo.

Alisema
mazoea na tabia ya kuweka fedha kwenye vitanda , kuchimbia chini au
kwenye mazizi ya mifungo ilishapitwa na wakati kwa kipindi hiki na
kuwataka vipato vyao vya pesa wanapopata kwenda kuziweka benki na
kwenye taasisi za zinazotunza fedha.

“Ndugu zangu wananchi uhai
katika maisha yetu ni bora sana, katika familia zetu , tabia ya
kuendelea kukaa na fedha majumbani kwetu ni hatari sana kwa sababu
unaweza kuvamiwa na watu waharifu wakawashambulia na kupoteza maisha
kwa hiyo rai yangu mnapopata pesa iwe hata kidogo lazima tupeleka
kuziweka benki,, Alisema Eng.Luhumba.

Eng. Luhumba katika hotuba
yake alitoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Mbogwe kutumia fursa
zinazotolewa na benki hiyo kujiletea mafanikio kiuchimi katika maisha
yao na kuwataka kuwa wakopaji wazuri wa mikopo na kulejesha kwa wakati.

Mbali na kuipongeza menejimenti ya benki hiyo, aliipa
changamoto ya kuhakikisha inaweza kuandaa Kongamano la biashara katika
mkoa wa Geita ilikuwapa msasa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla
kuhusu kuchangamkia fursa zilipo mkoani humo ilikuhakikisha wananchi
wanapata maendeleo yenye tija ndani na nje ya kanda ya Magharibi na
Afrika Mashariki.

Mkuu wa wilaya ya Mbogwe Martha Mkupasi alisema
anaishukuru benki ya NMB kwa kuwasogezea huduma za kibenki kutokana na
kuwa wananchi walikuwa na kilio cha siku nyingi kwa serikali kuitaka
benki kwa sababu walikuwa wasafiri zaidi ya kilimita 50 kufaata huduma
hizo wilaya jirani za Bukombe na Kahama mkoa wa Shinyanga.

Mkupasi
alisema kufunguliwa kwa tawi hilo la benki hiyo kumewaondolea aza
waliyokuwa wanaipata kusafiri na fedha umabari mrefu hali iliyokuwa
inahatarisha maisha yao kwa kuhofia kuvamiwa na majambazi , kwa
kusogezewa huduma hiyo na kuwahimiza kutumia fursa hiyo kuichumi na
kujiletea maendeleo.

Awali katika hotuba yake mkuu wa kitengo cha
biashara wa benki ya NMB , Donatus Richard alisema sasa tawi hilo ni
la 229 kwa nchi zima na huo ni wajibu wao katika kuwasogezea huduma
hizo wananchi, wafanyabiashara wa dogo, wa kati na wakubwa ili
kuwawezesha watu kupata mitaji kwa ajili ya biashara na shughuli
mbalimbali nalengo la kuwanyanyua kiuchumi na kuwaomba wachangamikie
fursa zionazotolewa na benki ili kujiletea maendeleo.

Share.

About Author

Leave A Reply