Tuesday, July 23

BARAZA LA KILIMO TANZANIA LAENDELEA NA UJENZI NA UKARABATI WA MAGHALA MKOANI KATAVI.

0Tuesday, November 06, 2018

ZAIDI
ya wakulima 57,000 Mkoani Katavi wanatarajiwa kunufaika na mafunzo
yatakayowasaidia kuongeza uzalishaji katika mazao yao, namna bora ya
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kujengewa
uwezo wa namna ya upatikanaji wa masoko kwa mazao wanayolima.

Aidha
pia imeelezwa kuwa ili kuendelea kuinua kiwango cha uzalishaji kwa
wakulima mkoani humo zaidi ya maghala 18 ya kuhifadhia mazao
yanatarajiwa kujengwa hasa katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa
mazao,

Hayo yalielezwa na Afisa Biashara kutoka Baraza la
Kilimo Tanzania Bw Alinanuswe Ambalile Mkoani Katavi na kusema kazi
kubwa katika Mkoa huo imekwisha kufanyika hasa katika kuwajengea uwezo
wakulima wadogo ili kuongeza thamani mazao yao.

Bw Ambalile
alisema kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2018/19 Baraza la Kilimo Tanzania
kwa kushirikiana na Mradi wa TIJA TANZANIA wanatarajia kujenga
mashamba darasa zaidi 42 kwa mazao ya Mahindi, Mpunga na Maharage,lengo
ikiwa ni kuendelea kumjengea uwezo mkulima.

“Baraza la kilimo
Tanzania linafahamu msimu wa kilimo umekaribia na tayari tumekwisha
kukarabati maghala 7 ya kuhifadhia mazao pia tumekwisha kuwajengea
uwezo wakulima ili mazao wanayozalisha yaendane na mahitaji ya soko na
tunaamini kupitia mabadiliko haya tunayoyafanya katika kuweka mashamba
darasa hayo 42 wakulima watakuwa na uwezo mzuri zaidi wakulima kilimo
chenye tija” alisema Bw Ambalile.

Muonekano
wa Ghala la kuhifadhia mazao linalojengwa na Baraza la Kilimo Tanzania
chini ya udhamini wa AGRA katika Kijiji cha Mnyagala Mkoani Katavi
likiwa katika hatua za mwisho za kukamilika kwake ambapo baada ya
kukamilika litakuwa na uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 660. 

Mafundi
wakiendelea na hatua za uwekaji Kenki katika ghala hilo ambalo
litawasaidia wakulima wa kijiji hiki cha Mnyagala ambao ni wakulima
wakubwa wa Mpunga mkaoni Katavi kuwa na uwezo wa kuhifadhi mazao yao,
ghala hili linatajwa kuwa la kisasa la kipekee katika kijiji hicho.

Mafundi
wakiendelea na hatua za mwisho za ukarabati wa Ghala la kuhifadhia
mazao la kampuni ya Nondo Investiment iliyoko Mkoani Katavi, Ukarabati
ambao unaratibiwa na Baraza la Kilimo Tanzania chini ya udhamini wa AGRA
ambapo baada ya ukarabati huo kukamilika ghala hilo litakuwa na uwezo
wa kuhifadhi tani 10000.

Muonekano
wan je wa ghala hilo baada ya kufanyiwa marekebisho kwa kuongeza urefu
wa ghala hilo ambapo awali lilikuwa na uwezo wa kubeba tani 7000 pekee
lakini baada ya kukamilika kwake litakuwa na uwezo wa kubeba tani 10000,
ukarabati wote huo unafanywa na Baraza la Kilimo Tanzania chini ya
udhamini wa AGRA.

Mafundi
wakiwa katika hatua za mwisho za uwekaji wa kenki katika ghala jipya
linalojengwa na Baraza la Kilimo Tanzania katika Kata ya Mishamo Mkoani
Katavi ambapo baada ya kukamilika kwa ghala hilo litakuwa na uwezo wa
kuhifadhi zaidi ya tani 660 za mazao.

Share.

About Author

Leave A Reply