Monday, August 19

AJALI YAUA WATU 2 NA KUJERUI WENGINE 5 ARUSHA

0


Na. Vero Ignatus Arusha

Watu wawili wamefariki na watano kujeruhiwa, katika ajali iliyotokea majira ya saa tisa alasiri, katika barabara itokayo Arusha kwenda Namanga, eneo la Oldonyosambu ambapo imeusisha magari mawili madogo toyota T612 saloon na Mitsubish saloon KCH 665

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shanna amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema chanzo chake ni uzembe na mwendo kasi. 

” Dereva wa gari la dereva wa gari ya nyuma alikuwa anakata kona kuelekea ngarenanyuki mkono wa kulia na gari ya nyuma ikaovatake mkono wa kulia ndipo yakagongana. Amesema Kamanda Shanna ” 

Kamanda Shanna amewataja waliofariki ni dereva aliyetambuliwa kwa jina la Onesmo Machia Mwangi miaka 20 ni mfanyabiashara raia wa Kenya na mwingine aliyetambulika kwa jina moja la Hendry

Amesema majeruhi wote wanatibiwa katika hospitali ya Serilani Ngaramtoni ila hali zao bado ni mbaya.

Aidha amesema Jeshi la Polisi halikubaliani uzembe wowote unaofanywa na madereva wakiwa barabarani na ametoa onyo kwa madereva ambao wanaendesha magari wakiwa wamelewa sheria itachukua mkondo wake. 

Share.

About Author

Leave A Reply