Monday, June 17

MAJAMBAZI YASHAMBULIA KWA RISASI BASI LA MAGEREZA NA KUTOWEKA NA MAHABUSU ALIYEKUWA KATIKA BASI HILO

0


 Wananchi katika eneo la Mayfair, Mikocheni jijini Dar es Salaam, wakitazama basi la Magereza lenye namba MT 0046, lililoharibika kwa kusambaratishwa baadhi ya vioo, katika barabara ya Old Bagamoyo, baada ya kushambuliwa kwa risasi na majambazi yasiojulikana ambayo yalifanikiwa kutoweka na mahabusu mmoja aliyekuwa miongoni mwa mahabusu waliokuwa wakisafirishwa kwa basi hilo leo. Katika tukio holo, mahabusu wawili na askari mmoja wa Magereza wamejeruhiwa.

 sehemu ya nyuma ya basi hilo ikiwa wazi baada kioo kusambaratishwa kwa risasi na majambazi hayo kufanikiwa kumtorosha mahabusu kupitia sehemu hiyo.

Kikundi cha Ngoma cha Rugu- Karagwe chatwaa ubingwa wa Mkoa Balimi Ngoma Kagera.

 Baadhi ya wacheza ngoma wa kikundi cha Rugu kutoka Karagwe mkoani Kagera wakishangilia na kitita cha Shilingi 600,000/=mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Balimi Ngoma Mkoa wa Kagera yaliyofanyika katika Uwanja wa Kaitaba Bukoba mjini.
Baadhi ya washiriki na mashabiki wa Balimi Ngoma wakishuhudia fainali za mashindano ya Ngoma mkoa wa Kagera yaliyofanyika  katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mjini.

Na Mwandishi Wetu.
FAINALI za mashindano ya Ngoma za Asili  ngazi ya mikoa zijulikanazo kama “Balimi Ngoma Festival 2014” Mkoani Kagera kikundi cha Rugu chenye makazi yake Karagwe kimefanikiwa kuwaa ubingwa wa Mkoa wa Kagera  na kuzawadiwa fedha taslimu Shingi 600,00/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Kagera katika fainali za Kanda zinazotarajiwa kufanyika Augusti 16,2014 Mkoani Mwanza.
Nafasi ya pili ya mashindano hayo ilichukuliwa na Kikundi cha Rugoloile cha mjini Bukoba ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa katika fainali za Kanda.
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Abagambakamo cha Muleba  ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= na nafasi ya nneilichukuliwa na kikundi cha Alute Continue ambacho kilizawadiwa fedha taslimu shilingi 300,000/=.
Nafasi ya tano mpaka ya mkumi ilichukuliwa na Uviti Ruzinga,Chupukizi,Kasharu,Kabete cha Ihangilo,Jipe Moyo na Upendo Musira hivi vilizawadiwa kifuta jasho cha 150,000/= kila kikundi.Jumla ya Vikundi 11 vilijitokeza kushiriki fainali hizo za Mkoa wa Kagera ngazi ya Mkoa kwa Mwaka 2014.
Akizungumza na kwa nyakati tofauti Meneja matukio wa Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela alisema Sababu msinigi ya kuwepo kwa Mashindano ya Balimi Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania.
Mwayela aliongeza pia kuwa wao Kampuni ya Bia nchini ni sehemu yao ya kurudisha fadhila kwa watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra Lager pamoja na vinywaji vyote vya Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).
Fainali za Mkoa wa Kagera zilifanyika katika Uwanja wa Mkoa wa Kaitaba na fainali za Kanda za mashindano ya Balimi Ngoma zinatarajiwa kufanyika August 16,2014 jijini Mwanza kwa kushilikisha vikundi viwili viwili kutoka Tabora, Shinyanga, Bukoba,  Musoma na Wenyeji wa mashindano Mwanza.

MFARANSA SEAN GARNIER AJA TANZANIA KUONYESHA UMAHIRI WA KUCHEZA MPIRA WA MTAANI HUKU AKIBINUKA SARAKASI NA KUCHEZA DANSI

 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya kimichezo akifafanua machache mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa. Pembeni yake kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Mohn’s John Ntuli na Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi.

  
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha staili mbali mbali za kucheza mpira mbele ya waandishi wa habari.
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha jinsi ambavyo unaweza kupiga danadana huku ukiwa unacheza mziki staili mbali mbali.
  Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha jinsi ambavyo unaweza kupiga danadana na kupita katika tundu dogo huku ukiendelea na mchezo. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa leo anatarajiwa kuonyesha shoo ya bure ambapo ataonesha umahiri wa kucheza mpira wa mitaani, sarakasi na kucheza dansi.
Mfaransa huyo Sean Garnier ambaye yuko nchini kwa ziara maalum ya kimichezo jana usiku alianza ziara hiyo kwa kuonesha umahiri wake wa kucheza mpira wa mtaani katika viwanja vya ufukwe wa Coco (Coco Beach) jijini Dar es Salaam.
Garnier ambaye anakipaji cha kupiga danadana mpira huku akiweka mapozi mbalimbali alionekana kuwa kivutio mbele ya mkutano na waandishi wa habari ambao walikuwepo kwenye mkutano huo huku akionesha umahiri wake wa kupiga danadana na kucheza na mpira katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi baada ya mkutano huo.
Mwenyeji wa ziara ya Garnier, Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi alisema kwamba huyu ni mwanamichezo mwenye kushikilia taji la kipaji cha kucheza ‘Free Style’ duniani.
“Ameletwa kwa udhamini wa ‘Redbull Street Sytle’ na atakuwa nchini kwa siku tano ambapo ni kati ya Julai 2 hadi Julai 7 ataondoka.
Aidha mbali ya kumudu kucheza na mpira pia nacheza sarakasi katika mitindo mbalimbali huku akiwataka watanzania kuiga baadhi ya michezo ambayo ataionyesha akiwa atakapokuwa mtaani.
Baadhi ya mitaa atakayo pita ni Kariakoo, Mlimani City, Posta, Viwanja vua Sabasaba, Chuo Cha Biashara (CBE) na Sea Clif Jijini Dar es Salaam.Read More

Share.

About Author

Leave A Reply