Sunday, August 25

CCM YAANZA KUMTANGAZA MGOMBEA WAKE WA URAIS DK. JOHN MAGUFULI MJINI DODOMA.

0


 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi John Pombe Magufulu pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwasalimia wananchi waliojitokeza kwenye uwanja wa  Jamhuri mjini Dodoma  Dk. Magufuli akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi kuja kumsalimia na kumuona mgombea huyo wa CCM.
Dk. Magufuli akisalimiana na wananchi
 Mgombea mwenza wa Dk. Magufuli, Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wa Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Dk. John Magufuli akizungumza na wakazi wa Dodoma ikiwa sehemu yake ya kwanza  kujitambulisha kwa wananchi baada ya kutangazwa kuwa mgombea rasmi wa CCM.

DK. JOHN MAGUFULI MGOMBEA RASMI WA URAIS KWA TIKETI YA CCM, AMTEUA SAMIAH SULUHU KUWA MGOMBEA MWENZA WAKE. 

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jaaya Kikwete akionyesha kuwa mwenye furaha isiyo kifani baada ya Dk. John Magufui (kulia)  kutangazwa kuwa mshindi, na hivyo kupata ridhaa ya kupeperisha bendera ya CCM kaika uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka huu.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha jukwaani, Mke wa Dk. John Magufuli, Mama Janeth Magufuli
“Hili jembe” akisema Rais Kikwete wakati akiwa na Dk. John Maguli na Mama Janeth Magufuli baada ya matokeo ya uchaguzi wa kumpata mgombea wa CCM yaliyotangazwa na Spika wa Bunge Mama Anna Makinda leo mjini Dodoma
Rais Kikwete akionyesha zaidi furaha yake
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto) akiwa na Mama Janeth Magufuli, huku Rais Kikwete akiendelea kufurahi
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimpongeza Dk. Magufuli
 
KABLA YA MATOKEO KUTANGAZWA
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wajumbe na wageni waalikwa baada ya kuwasili katika Ukumbi wa kisasa wa mikutano mjini Dodoma leo kwa ajili ya shughuli ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa kumpata mgombea Urais kwa tiketi ya CCM ambao ulifanyika jana usiku.Kushoto ni Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu Mwenyekiti wa CCM Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete baada ya kuwasili katika Ukumbi wa kisasa wa mikutano mjini Dodoma leo kwa ajili ya shughuli ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa kumpata mgombea Urais kwa tiketi ya CCM ambao ulifanyika jana usiku.Kushoto ni Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu Mwenyekiti wa CCM Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiiti wa CCM Bara, Phlip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihamasisha wajumbe  ukumbini wakati wakisubiri kutangazwa matokeo hayo
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi akisoma taaifa ya serikali, kabla ya kutangazwa matokeo hayo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akijadiliana jambo na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein wakati yakisubiriwa kutangazwa matokeo hayo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akieleza utekelezaji wa serikali wa ilani ya CCM wakati yakisubiriwa kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdurahman Kinana wakitafakari mambo mbalimbali wakati wa kusubiri kutangazw amatokeo ya mgombewa urais kwa tiketi ya CCM katika uchagzi mkuu utakaofanyika mwaka huu
Mwimbaji Ali Star akiimba wimbo maalum wa CCM wakati wa shamrashamra a kusubiri matokeo hayo
Wajumbe na waalikwa wajikimwayamwaya ukumbini wakati wakisubiri matokeo hayo
Katibu Mkuu wa CCM mstaafu Mzee Wilson Mukaa akifuatilia hali ya mambo yalivyokuwa ukumbini wakati yakisubiriwa matokeo hayo
Spika wa Bunge Anna Makinda na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, wakimkabidhi leo Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete matokeo ya uchaguzi wa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM uliofanyika jana usiku
Spika wa Bunge Anna Makinda akitangaza matokeo hayo baada ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete kuyahakiki
Mgombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu, kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli (kushoto) wakati akisubiri kutangazwa kwa matokeo hayo
Walinzi wa usalama,  wakiwa wamemzunguka Dk. John Magufuli mara matokeo yalipoonyesha kuwa ameshinda na hivyo kuwa mgombea rasmi wa Urais kwa tiketi ya CCM leo
Dk. Magufuli akiwa ‘amezongwa’ na walinzi waliokuwa wakimpeleka jukwaani baada ya kuytangazwa kuwa ndiye mshindi
Dk. Magufuli akiwa ‘amezongwa’ na walinzi waliokuwa wakimpeleka jukwaani baada ya kuytangazwa kuwa ndiye mshindi
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsubiri kwa hamu Dk. John Magufuli wakati akipanda jukwaani
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akimkubatia kumpongeza Dk. Magufuli kwa kupata ushindi
Rais Kikwete akizidi kumpongeza Dk. Magufuli
“wewe ni jembe letu” akasema Rais Kikwete
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimnadi kwa wajumbe Dk. Magufuli baada ya kutangazwa mshindi
Dk. Magufuli akimshuku Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein kwa jinsi Chama kilivyosimamia uchaguzi na kumalizika salama
Dk. Magufuli akimsalimia Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpongeza Magufuli
Baadhi ya wadau ndani ya ukumbi wakati wa kutangazwa matokeo hayo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza kwa furaha, Mama Janeth Magufuli
Aliyekuwa akiomba ridhaa ya CCM kuwania Urais, Mwigulu Nchemba naye akiungana na wadau kufurahia Dk. Magufuli kuibuka mshindi

BAADA YA MAGUFULI KUWA MGOMBEA RASMI KWA TIKETI YA CCM
 Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein akitoa maelezo alivyjipanga kuongoza tena mhulamwingie, kufuatia kuteuliwa tena kuwa mgombea wa Urais wa zanzibar kwa tiketi ya CCm katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu
 Aliyekuwa mgombea wa kupata ridhaa ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Asha Rose Migiro akitoa shukrani zake, wakati wa kutangazwa matokeo ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM na yeye kuibuka watatu kutokana na kupata kura chache Kushoto ni mumewe, Profesa Migiro
 Aliyekuwa mgombea wa kupata ridhaa ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM Balozi Amina Ally akitoa shukrani zake, wakati wa kutangazwa matokeo ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM na yeye kuibuka wapili kutokana na kupata kura chachedhidi ya Dk. Magufuli
  Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, Dk. John Magufuli, akitoa maelezo yake alivyojipanga kuongoza nchi, baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kupata nafasi hiyo matokeo ya uchaguzi uliofanyika jana usiku yalipotangazwa leo
  Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu, Dk. John Magufuli, akimnadi Mgombea wake mwenza, Samiah Suluhu, baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kupata nafasi hiyo matokeo ya uchaguzi uliofanyika jana usiku yalipotangazwa leo
 Samiah Suluhu akitafakari baada ya kuteuliwa na Dk. Magufuli kuwa mgombea wake mwenza
 Kisha akaonyesha furaha yake ya kuteuliwa huko kuwa mgombea mwenza
 Mama Janeth Magufuli akimpongeza samiah Suluhu. Kulia ni Mama Mwanamwema Shein
 Mama Salma Kikwete akiungana na Spika wa Bunge Mama Anna Makinda kumpongeza Samiah Suluhu
Mweneyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akiufunga Mkutano Mkuu maalum, baada ya shughuli ya kutangaza matokeo ya mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM kumalizika leo, mjini Dodoma
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwapongeza Dk.Magufuli na Samiah Suluhu baada ya kuufunga mkutano huo.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na baadhi ya viongozi wa meza kuu, wakiwa katika picha ya pamoja na Dk, Magufuli na Samiah Suluhu baada ya kufunga mkutano huo
 Rais Mstaafu Ali Hassani Mwinyi akiondoka ukumbini huku akiwa amemshika mkono Dk. Magufuli. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-theNkoromo Blog  Read More

Share.

About Author

Leave A Reply