Saturday, August 24

Ushirikiano kati ya HaloPesa na VISA wazinduliwa

0


Mwezi Novemba mwaka jana zilitoka taarifa kuhusu ushirikiano kati ya VISA na Halopesa na hapa ni dhahiri shahiri suala hili linahusisha masuala ya miamala ya fedha kati ya pande mbili zinazohusika. Suala hilo sasa ni rasmi baada ya wahusika kusaini hati ya makubaliano.

Watanzania wanaianza wiki ya Mei 20 2019 kwa tabasamu hasa kwa wale ambao ni wateja/watumiaji wa HaloPesa lakini pia mteja wa benki ambae anafanya miamala mbalimbali kwa njia ya simu. VISA na HaloPesa kwa pamoja wameamuakutanua wigo wa biashara kwa kuamua kurahisisha njia ya kidijiti kufanya malipo/miamala ya bidhaa mbalimbali.

Nini maana ya makubaliano kati ya pande mbili zinazohusika?

Mteja yeyote wa HaloPesa kupitia VISA atapewa msimbo (QR code), namba ya wakala wa HaloPesa na aliyesajiliwa kufanya miamala kwa VISA kisha mteja kutumia simu janja kulipia/kufanya muamala baada ya shughuli ya kufichua msimbo kukamilika na malipo kufannyika.

Ushirikiano kati ya HaloPesa

Majaribio ya kufanay malipo kwa kupitia VISA kutoka HaloPesa yaliyohududiwa na Meneja wa VISA Tanzania (wa pili kulia).

Suala hilo pia lina maanisha wateja wa HaloPesa wataweza kupata kufanya miamala kwa wepesi kwani mpaka sasa kuna mawakala wa HaloPesa zaidi ya arobaini elfu (40,000) huku wateja wa huduma hiyo wakifikia 1.3M mpaka mwisho wa mwaka jana.

Ushirikiano kati ya HaloPesa

Hafla ya kuweka saini kati ya HaloPesa na VISA iliyowahusu Meneja wa VISA Tanzania, Bi. Olive Njoroge (kushoto) na Naibu Mkurugenzi wa Hakotel, Bw. Nguyen Tien Dung (kulia).

Vipi unaamini ushirikiano huu utatanua wigo wa biashara kati ya pande hizo mbili hasa ukizingatia Halotel ndio wa kwanza kujitosa ulingoni na kuwaleta watu karibu na VISA kupitia HaloPesa? Tuambie maoni yako hapo chini.

Vyanzo: The Habarii, Gazeti la The Citizen

Share.

About Author

Leave A Reply