Tuesday, August 20

LG na muundo wa kamera tatu za mbele kwenye simu

0


vodacom swahili

miaka ya karibuni sio rahisi kuona simu janja mpya ilitoka ikiwa haina kamera ya mbele na hii ikitokana na ukuaji wa teknolojia lakini pia hata watumiaji wenye kupenda picha za ‘Kujipiga mwenyewe’.

LG (Life’s Good) wanaonekana wanataka simu zao zijazo ziwe za kitofauti na washindani wengine kwa kuamua kwenda kusajili muudo wa kamera tatu kwenye simu janja kabla ya mtu (kampuni) mwingine yeyote. Jambo hilo liliweza kufanyika na wakafanikiwa kutambulika kama kampuni ambayo ina miliki mchoro wa simu wenye muudo tofauti kwa kamera za mbele.

Muonekano+Mpangilio wa kamera

Kwa muonekano hautofautiani sana na LG V50 na pengine hii ikimaanisha muundo huo huenda ikawa ni kwa simu zinazofuata baada ya toleo la sasa (LG V50). Kwenye kamera  za mbele ambazo zitakuwa tatu kwa idadi; ile ya kwanza itakuwa na lenzi ya kiwango cha juu, ikifuatiwa na sensa mahususi kwa ajili ya kufanya picha iwe pana na ya mwisho hunda ikawa ya ToF (Time of Flight).

Upande wa kushoto kuna vitufe vya kupunguza/ kuongeza sauti, kitufe cha Google Assistant. Ukiangalia upande wa kulia utaona kitufe cha kuzima/kuwasha simu, sehemu ya kuweka laini za simu, memori ya ziada. Upande wa juu hakuna kitu chochote na kwa nyuma ni kamera tatu pamoja na teknolojia ya kutumia alama ya kidole.

kamera tatu

Muudo wa toleo lijalo la simu janja za LG: Inaonekana kuwa simu hizo pia hazitakuwa na sehemu ya kuchomeka spika za masikioni.

Suala zima la wizi wa ubunifu wa muundo linasumbua makampuni mengi na ndio maana mara tu baada ya kukamilisha mchoro wanapelekwa kwa mamlaka husika ili kuweza kutambulika kuwa mchoro huo ni wa kwao hivyo basi kuwez kupewa haki ya umiliki.

Share.

About Author

Leave A Reply