Saturday, August 17

Instagram kuficha idadi ya watu waliopenda chapisho

0


vodacom swahili

Instagram imekuwa ni sehemu ya baadhi ya watu kuweza kujiingizia kipato kutokana na kujulikana kwao kwa jamii hivyo kuleta mawasiliano baina ya watu na machapisho mbalimbali bila kusahau idadi ya watu walioona/kupenda chapisho fulani.

Kwenye Instagram sio kitu cha ajabu kuona chapisho limependa na mamia kwa maelfu ya watu na hii inatokana na kuvutia kwa kile ambacho mhusika amekiweka huko ili watu waweze kuona na kwa wengine idadi ya watu wengi waliopenda chapisho ndio kivutio cha kupata matangazo ya biashara kutoka kwa makampuni watu mbalimbali.

Instagram wanafikiria kufanya kitu ambacho kinaweza kispendwe na watu ambao walikuwa wanapata kazi kutokana na idadi ya watu waliotokea kupenda chapisho; huenda Instagram ikaficha kuonyesha idadi ya watu waliotokea kuvutia na kitu fulani kwenye akaunti ya mtu sababu ni kutaka wale watu watiliemaanani zaidi kile kilichochaposhwa kuliko idadi ya watu walitokea kupenda picha/picha mnato iliyowekwa.

Lakini pia Instagram wanataka kuwapunguzia watu hofu kutokana na idadi kubwa/ndogo ya watu waliotokea kupenda kitu fulani kitu ambacho kinaweza kusababisha uraibu/msongo wa mawazo.

waliopenda chapisho

Maboresho kwenye Instagram: Instagram kuficha jumla ya watu waliopenda chapisho lakini kuonekana kwa aliyechapisha.

Basi tumeshakutaarifu usije ukashangaa unaperuzi kwenye Instagram na usionene idadi ya jumla kwa watu waliotokea kupenda chapisho fulani (iwapo chapisho husika halijawekwa kwenye akaunti yako). Jambo hili linaweza kuchukiza/kufurahisha wengi?

Share.

About Author

Leave A Reply