Tuesday, August 20

UHUSIANO KATI YA DAMU NA TABIA

0


Je unajua kuwa tabia ulizonazo ni kutokana na kundi lako la damu?
Kwa kawaida kila binadamu yuko kwenye kundi mojawapo la damu kati ya makundi manne A,B,AB na O. Makundi haya yanaweza kutumika kufahamu tabia za binadamu na jinsi hii yaweza kuwa rahisi na ya karibu zaidi kuliko kutumia nyota “astrology” kama ambavyo wengi wanafanya, na wataalamu wanasema tabia kwa uhusiano na kundi la damu ina uhakika zaidi kuliko wenye vyanzo vingine. Mbali na tabia, ukweli ni kwamba makundi yetu ya damu yanaweza kutuonyesha pia vile mtu anavyopendelea na asivyopendelea, kazi anazopendelea, watu anaowapendelea na hata vyakula. Baadhi ya watafiti nchini korea wamebainisha kuwa hata namna tunavyopendelea kuketi hutegemea sana na makundi yetu ya damu, sasa tuangalie uhusiano huu
Damu kundi “A”
Hawa watu maranyingi huwa mifano ya kuigwa na wengi kwasababu ya kiu zao na upiganaji wao kwenye mafanikio, ni watu wema,wapole na wenye tabia njema. Pamoja na hayo ni rahisi sana watu hawa kupata msongo wa mawazo “stress” na kufikiria sana vitu. Wakiamua kujitoa kwa ajili ya kumsaidia mtu basi wanazama kabisa na wanaweza hata kujisahau wao.
Mazuri yao
 • Ni watu wanaopenda vitu vikamilike katika hali ya juu “perfectionists”, wanapenda mpangilio maalumu, wanapenda na wanaweza kuchambua mambo sawia, wanawajibika na kubeba majukumu yao,wana huruma na wako tayari kusaidia, waaminifu, ni wagunduzi, wanamaanisha, wavumilivu, na wenye tabia njema.
Mapungufu yao
 • Wasumbufu,wana hisia kali hata kwenye vitu vya kawaida, wakitaka kitu wametaka, wengine wana aibu,wengine wakimya zaidi na wanaopenda kujichanganya.
Kwenye maisha ya kijamii
 • Ni mtu ambaye unaweza kumwamini na kumtegemea
 • Anajali na kumaanisha
 • Wakati wote huepuka shari,misuguano na magomvi
 • Maranyingi hawapendezwi wala kufurahia sherehe zenye makelele na shangwe za ajabu ajabu,wanapendelea ukimya na utulivu.
Kazini
 • Unaweza kumwamini na kumtegemea katika majukumu
 • Wanapenda ufanisi wa kiwango cha juu kwahiyo kazi zao mara nyingi ni bora sana.
 • Bahati mbaya wanajali sana hata vitu vilivyo vidogo nahii huwafanya kuwa na msongo wa mawazo kirahisi.
 • Wasio waelewa vema watu wa kundi hili wanaweza kupata shida kufanya nao kazi
Kwenye mahusiano na mapenzi
 • Ni ngumu kidogo wao kufunguka na kushirikisha mambo yao.
 • Wanaweza kuonekana wenye aibu, au waoga.
 • Ukitaka kumchumbia au kuchumbiwa na mtu wa kundi ‘A’ unahitaji uvumilivu.
 • Wakiamua kupenda utawafahamu wakati wote na ingawa watakuruhusu ufahamu tu yale maeneoa ya maishani mwao ambayo wanajua unahusika, hawawi wazi katika kila eneo.
Ukweli mwingine kuhusu watu wa kundi ‘A’
 • Ni watu wabunifu na wenye ujuzi wa usanii “artists”
 • Wanalewa kirahisi sana, kilevi kidogo tu kitampelekesha sana
 • Wengi wao hupendelea kula mboga mboga “vegetarians”
Damu kundi “B”
Watu wa kundi hili maranyingi ni wenye tabia za kuasi na ni ngumu kuwazuia au kuwatuliza. Wanandoto na maono makubwa,wanasukumwa kwa kasi na kiu zao ingawa wanaweza kuwa wakali na wasumbufu na mara nyingine ngumu kukaa na kuzoeana nao. Wanakisimamia sana kile wanachokiamini hata kama ulimwengu mzima usimame kinyume nao.
Mazuri yao
Wanasukumwa  katika kufikia malengo yao, wako kasi kiutendaji,wanapenda raha,wana hisia nzito , wanayatazama maisha katika mtazamo chanya , wanaweza kujisimamia na kujitegemea na hawahitaji ushirika au kukubaliwa na wengine.
Mapungufu yao
Wabinafsi sana,mara nyingine wanakwepa majukumu yao,wagumu sana kusamehe,wasumbufu,wanaweza kuwa wakatitili na wenye hasira za haraka.
Maisha yao kijamii
Maranyingine ni ngumu kushirikiana nao au kuwa nao maana wanapenda kufanya mambo yao wenyewe.
Kazini
Ingawa  wanaweza kuwa na malengo mengi na maono pia lakini wanaweza kuwa wasumbufu na wagumu katika kushirikiana nao kazini. Ni ngumu kufanya nao kazi maana wanataka kufanya pekeyao.
Mahusiano na mapenzi
 • Unaweza kufurahi nao sana kwenye mapenzi lakini uwe tayari kuvumilia hasira zao kali na za ghafla. Vumilia hali yao ya kukwepa majukumu pia,fahamu kuwa wanaweza kuwa wakali, wakatili na wasio maanisha kile wanachokisema.
Baadhi ya ukweli wa kitafiti kuhusu watu wa kundi B
 • Wanatabia ya utukutu.
 • Pamoja na baadhi ya mazuri yao bado wanaweza wasiwe watu wazuri kwenye kuwa mume, au kuwa wapenzi wazuri kwa wasichana wao. Hii ni kutokana na urahisi wa tabia za kukosa uaminifu kimapenzi na urahisi wa kuumiza mioyo ya wengine.
 • Wanatabia ya kupenda wanyama “they love pets”
 • Wana kinga kubwa na imara ya mwili katika kujikinga na magonjwa.
 • Wanafurahia zaidi vyakula vitokanavyo na wanyama kama vile maziwa “dairy products” n.k
Damu kundi   “AB”
Kundi hili ni watu wenye haiba mchanganyiko, hawa huwa na tabia tofauti kuanzia kuwa waoga na wenye aibu hadi wengine ni wapenda mitoko na wacheshi,wako wanafanya mambo kwa kuongozwa na mawazo na wengine hawawazi kabisa kile wanacho taka kukifanya,hii inafanya watu wa kundi hili kuwa watu wa kushangaza sana mara unapokuwa nao.
Mazuri yao
 • Ni rahisi sana kuwa rafiki nao.
 • Wanachukuliana na mazingira haraka na kwa urahisi.
 • Wenye kufurahisha unapokuwa nao ingawa ni watu wasiotabirika.
 • Wana mawazo,wana akili sana,hupenda kuweka mambo yao kwa vitendo na pia huongozwa na misimamo ya kifikra.
Mapungufu yao
 • Wagumu katika kufanya maamuzi.
 • Wanasahau sana
 • Ni wenye hisia za kayumba “mood swing”, mara wana furaha mara wamekasirika.
 • Sio waaminifu.
 • Ni wapinzani,wabishi na wakosaji.
 • Ni watu wabinafsi.
Maisha ya kijamii
 • Wanaweza kuwa marafiki wazuri na wenye kufurahisha.
 • Maongezi yao ni yenye kuhamasisha nayenye akili na kufikiria kwa hali ya juu.
 • Kwa kutokuwa wenye kutabirika, wengine huhofia kuumizwa kihisia au kukatishwa tamaa au kuumizwa moyo na watu hawa, hususani pale wanapokuwa sio waaminifu.
Kazini
 • Wanaweza kuwafurahisha na kuwapa burudani mnapofanya kazi nao lakini sio watu wa kuwategemea sana,wanaweza kukuangusha kirahisi.
Mahusiano ya mapenzi
 • Kuwa katika mahusiano na mtu wa kundi la damu la AB kunaweza kuwa kwenye kufurahisha,unaweza usiwena nyakati nyingi za upweke. Pamoja na haya fahamu kwamba watu hawa wanaweza kuwa wabishi na wakosoaji na maranyingine maneno yao yanaumiza. Mpenzi wa mtu au watu wa hivi lazima aelewe jinsi hisia zao zilivyo na zinavyobadilika mara kwa mara,na pale inapobidi basi uwetayari kuwapa nafasi wanayostahili ili usijiumize sana.
Baadhi ya ukweli wa kiutafiti kuhusu watu wa kundi hili.
 • Ni watu wazuri kwenye mambo yahusuyo fedha.
 • Maranyingi wanajihusisha na wanaopendendelea shuhuli za kisanaa au mambo yenye sanaa ‘arts’
 • Ni watu wanaoaminika kuwa wabinafsi zaidi hata katika uchangiaji wa damu,watu hawa wanaweza kupewa damu na mtu mwingine yeyote ila wao hawawezi kumpa damu yeyote isipokuwa mwenzao wa AB.
 • Kama walivyo watu wa kundi ‘A’ na kundi ‘B’,watu wa kundi la damu ‘AB’ hupendelea vyakula vya mboga mboga “vegetables” na pia vyakula vitokanavyo na wanyama “dairy products”
Kundi la damu aina ya O
Hawa maranyingi wanajitahidi kuwa mahodari na mashujaa katika mambo tofauti. Mara zote kiu yao ni kuwafurahisha na kuwapendeza watu wengine ni wenye moyo wa uongozi wenye kiu ya kuwaona rafiki zao wakiwa wenye furaha wakati wote. Sio wagumu wa mabadiliko, wako tayari kubadilika, ni wenye mawazo mapana naya wazi, sio wagumu kifikra na ni marafiki wazuri.

Faida zao 
 • Ni wenye ujasiri, wanashindana katika mambo mengi mfano mambo ya maendeleo, hufanya kazi sana na kwa bidi, ni waaminifu, wanaweza kujieleza, ni marafiki wazuri, wanasamehe, mitazamo yao ni chanya, huweza kuhisi au kuonamambo hata kabla hayajatokea,wanakiu ya kufahamu na kudadisi na pia niwatu wema na watoaji.
Mapungufu yao
 • Maranyingine wanaweza kuwa wenye fujo, wanaopenda sifa, wanavutia vitu upande wao, wanaepuka au kukwepa majukumu,unaweza kuona hawa wanaigiza mambo, wakitaka wametaka hadi wapate na nirahisi kuwaondoa kwenye kile wanachokifanya “easy to be distracted”.
Maisha ya kijamii
 • Ni marafiki wazuri na unaoweza kuwategemea, ni waaminifu, ni wawazi,ingawa mara nyingine wanaweza kukuudhi, pia wakati mwingine wanatamani kusikilizwa wao tu.
Kazini
 • Wana kiu ya mafanikio, hufanya kazi kwa bidii ingawa kukatishwa tama na kupoteza hamasa ya kazi kirahisi sana. Mara nyingine ili wafikie malengo ni vema wakisimamiwa kwenye kazi wanayo fanya badala ya kuachwa wafanye wenyewe.
Mahusiano ya mapenzi
 • Ni watu wanaoweza kuonyesha mapenzi kwa wale wanaowapenda ila ni vema ukafahamu kuwa watu hawa hutarajia upendo wa jinsi ile ile wao wanavyoonyesha upendo kwako bila hivyo utakosana nao.
Ukweli wa kitafiti kuhusu watu hawa
 • Wanaaminika huwa na tabia za kijeshi.
 • Wengi wao kwa asili ni watu wa kupenda michezo.
 • Wanaaminika kuwa watu wema na waliotayari kusaidia mtu yeyote, hata katika uchangiaji wa damu ‘watu wa kundi ‘O’, wanaweza kumpa damu mtu mwingine yeyote.
 • Wanapendelea na kujisikia raha wanapokula nyama “meet lovers”.
Na: Dr. Chris Mauki ,Katika MASSHELE BLOG
Social, relationship and counseling psychologist
University of Dar es salaam
+255766605392Read More

Share.

About Author

Comments are closed.