Wednesday, August 21

TANGA RAHA SEHEMU YA 38

0


AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA


Jini la kiume ambalo ninaongea naye akaniishika mikono na gafla kufumba na kufumbua nikajikuta nikiwa katika anga na sikuamini macho yangu baada ya kuukuta mji mzima wa Tanga ukiwa umetawaliwa na damu nyingi lizilizo tapakaa maeneo mbalimbali ikiashiria watu wengi wametafunwa na majini yangu.

ENDELEA
Nikabaki nikihamaki kwani hali ilizidi kuwa mbaya,watu walikimbizama hovyo kuyaokoa maisha yao.Jini aliye nishika akanishusha juu ya gorofa moja la bandari.Kwa kutumia uwezo wa fimbo nilio nao nikaamaru majini wote kutulia,Wakatutii kwani maamlaka niliyo nayo juu yao yamezidi kuongezeka.Wakalizunguka eneo ambalo mimi nipo wakisubiri nini nifanye.
“Nani aliye waamuru kufanya huu upuuzi wakati niliwaachia kwa roo njema?”
Niliwauliza kwa ukali na majini wote wakaa kimya
“Aliye jijua kuwa amefanya tukio la kumla au kumdhuru binadamu yoyote ambaye ni mwema akae upande wangu wa kushoto”

Majini wakajigawa hadi mimi mwenyewe nikashangaa kwa jinsi wanavyo nisikiliza kwa umakini wa hali ya juu.
“Mkuu sisi ni wachache kati ya wale ambao wametekwa na wanadamu wenye nguvu zinazo endana na wewe.”
Jini mmoja alizungumza kwa sauti nzito akiwa katika kundi la majini walio watafuna watu.
“Hiyo sio mada niliyo nayo,nimeuliza ni kwanini mumewala watu wasio na hatia?”
“Mkuu wezetu ambao wametekwa walipandikizwa roho ambazo ni mbaya ndio maana wakawala watu na sisi tulio nusurika tukajua tumeruhusiwa kuwala watu ndio maana hata sisi tukawala”
Nikaangalia chini na kuona jinsi ukimya wa sehemu tuliyopo ulivyo tulia,Magari mengi yaliacha milango wazi huku mengine yakiwa yameangushwa na kuwashwa moto.
“KUMBUKA KUNA WATU WANAHITAJI MAJINI ILI KUYATUMIA KATIKA KAZI ZAO ZA KICHAWI NA WAGANGA,KUWA MAKINI NA HAO WATU.”

Sauti ya taratibu ilisikika masikioni mwangu,na ninauhakika hakuna jin lolote aliye weza kuisikia
“Sasa nifanye nini?”
“UNATAKIWA KUWAREJESHA KWANZA HAO 250 KAMA WALIVYO KISHA UANZE LILE AGIZO LA KWANZA ULILO PEWA.”
“Nitawarudisha vipi?”
“CHAGUA WAFUASI KUMI,NANE WAAMRISHE WAENDE KWENYE KILA KONA YA DUNIA WAKIWA WAWILI WAWILI,KISHA WAWILI WABAKI KATIKATI YA MKOA WAKO”
“Sijakuelewa,hao nane waende pende za dunia mzima au kwa huu mkoa tuiopo?”
“KWEENYE DUNIA,WANAKWENDA KUZUIA KUBADILISHWA KWA WEZAO,NA ENDAPO WEZAO WAKIBADILISHWA ZAIDI WATAWEZA KUKUANGAMIZA KWA MAANA WANAJUA SIRI ZAKO ZOTE”
“Sawa ila wewe sijajua ni nani?”
“MIMI UTANIJUA,NI KIONGOZI WAKO NILIYE AGIZWA KUFANYA KAZI HII”Read More

Share.

About Author

Comments are closed.