Monday, August 19

MWALIMU MKUU KAKONKO AJINYONGA AKIWA OFISINI MWAKE AACHA UJUMBE MZITO

0


MKUU wa Shule ya Sekondari Kakonko wilayani Kakonko mkoani Kigoma,Peter Rubonya amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba ofisini kwake mapema leo asubuhi.

Akielezea tukio hilo,Mwalim wa zamu wa shule hiyo Isaac Japhet amesema yeye alifika shuleni hapo saa 12:30 asubuhi ili kuwafundisha wanafunzi wa kidato cha nne masomo ya ziada baada ya kufunga shule wiki iliyopita na baada ya kufika aligundua kuwa hana chaki ambapo mkuu huyo wa shule alimpatia chaki mlinzi ili awape wananfunzi.

Amesema baada ya muda,Mratibu elimu kata pamoja na mmoja wa wazazi walifika ofisini hapo wakiwa na shida na mkuu wa shule na baada ya kuelezwa yupo ndani ofisini lakini baada ya kugonga mlango hawakuweza kujibiwa na ndipo wakaamua kufungua mlango na kukuta mwili wa marehemu ukining’inia dalini.

Mwalim Isaac amesema Mwalimu aliyejinyonga alikuwa akifundisha masomo ya Kemia na Fizikia shuleni hapo hawakuwahi kusikia mgogoro wowote wa kifamilia au kijamii, na mkewe ambaye ni mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM),alifika nyumbani kwake juzi akitokea Dodoma.

Kwa upande wa Mlinzi wa Shule hiyo Kajolo Kajabojabo amesema alikutana na Mkuu wa shule mapema asubuhi akiingia ofisini na kumuomba chaki ambazo alipewa na kuziwasilisha kwa walimu.

“Nilimuona kabisa tukasalimiana, nikamuuliza kama anaweza kuwa na chaki, akaingia ofisini akanipatia boksi moja la chaki.Nikachukua na kisha nikampelekea mwalim aliyehizihitaji, alikuwa kwenye hali nzuri tu, lakini baada ya muda ndo tukio hilo likatokea,”amesema Kajoro.

Akizungumza baada ya kufika shuleni hapo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kujua sababu ikiwa marehemu aliacha ujumbe wowote au laa.

“Hatujajua sababu lakini ni muhimu jamii ikajenga utamaduni wa kueleza matatizo ya ndani yanayoyasibu.Hiyo inasaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuepusha madhara kama haya,”amesema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Otieno amesema baada ya kupekuliwa kwa mwili wa marehemu walikuta karatasi imeandikwa ujumbe kuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Kakonko Lusubiro Mwakabibi asipodhibitiwa ataua wengi.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.