Monday, March 18

HII IKUFIKIE MWANA SIMBA KUHUSU BEKI MPYA SIMBA

0


Beki mpya wa Simba, Zana Coulibaly amefunguka kuwa hana wasiwasi wowote wa kuanza kuitumikia timu hiyo kwa kuwa bado anasubiria Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).

Coulibaly raia wa Burkina Faso, amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili katika usajili wa dirisha dogo unaotarajiwa kufungwa Desemba 15, mwaka huu.

Beki hiyo hakuweza kusafiri na timu hiyo kwenda nchini Eswatini katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows kutokana jina lake kutokuwepo kwenye michuano hiyo hali iliyosababisha kuachiwa programu maalum ya mazoezi binafsi.

Coulibaly alisema amekuwa akiendelea na ratiba aliyoachiwa na kocha wake na kwa sasa hawezi kucheza ligi mpaka itakapofika ITC yake.

“Unajua suala la lini nitaanza kuitumikia Simba kwangu siyo jambo kubwa kwa sababu bado naendelea na programu ambayo nimeachiwa na kocha ili niendelee kuwa sawa na kuendana na wenzangu.

“Nitacheza wakati ukifika kwa sababu Simba ni timu kubwa halafu ina wachezaji wazuri na kila mmoja ana nafasi ya kucheza lakini kwa upande mwingine bado ITC yangu haijafika na muda bado upo wa kutosha,” alisema Coulibaly.

Share.

About Author

Leave A Reply