Wednesday, June 19

Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Ataka Mashoga Wasitengwe

0


Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba mkoani Kagera, Desiderius Rwoma amekemea vitendo vya ushoga na kutaka wanaofanya dhambi hiyo wasitengwe na kubaguliwa badala yake wasaidiwe na kuonyeshwa ubaya wa wanachofanya.

Amesema kumvumilia mkosefu yeyote haina maana ya kumuunga mkono na kuwa ushoga ni dhambi na laana na watu wenye tabia hiyo wanahitaji msaada wa matibabu na huduma za kisaikolojia.

Katika mahubiri yake leo katika siku ya wanaume wa Jimbo Katoliki kwenye kanisa la Bikra Maria Mama wa Huruma, Askofu Rwoma ametaka uwepo wa sheria za kudhibiti vitendo vya ushoga

Share.

About Author

Leave A Reply