Saturday, August 24

WAZIRI WA MADINI AFUNGA MAONESHO YA MADINI DODOMA

0


Waziri wa Madini, Doto Biteko leo tarehe 27 Mei, 2019 amefunga Maonesho ya Madini ya siku mbili yaliyofanyika katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Maonesho hayo yaliyoanza tangu jana tarehe 26 Mei, 2019 yanahusisha Wizara ya Madini pamoja na Taasisi zake, Kampuni za Madini pamoja na wadau mbalimbali.

Lengo la maonesho hayo lilikuwa ni kutoa elimu kwa wabunge kuhusu Sekta ya Madini wakati wa uwasilishaji wa hotuba ya Wizara ya Madini.

Akizungumza wakati wa ufungaji wa maonesho hayo Waziri Biteko alieleza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imeanzisha kampeni ya miezi sita inayojulikana kama “Madini Yatatutoa” na kuandaa hafla ya “Usiku wa Madini” ambapo kampuni zinazofanya vizuri kwenye madini zitapewa tuzo kama njia ya kutangaza Sekta ya Madini.

Waziri Biteko mbali na kupongeza ushiriki wa Wizara pamoja na Taasisi zake, aliwahakikishia wachimbaji wa madini kuwa Serikali ipo tayari kuhakikisha wachimbaji wanafanya shughuli zao katika mazingira mazuri na kulipa kodi Serikalini.


Share.

About Author

Leave A Reply