Sunday, August 18

SERIKALI YATOA 92 BIL KUTATUA UHABA WA MAJI NYAMAGANA IFIKAPO 2020

0


Haya yamebainishwa na Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula wakati akijibu maswali ya Papo kwa Papo katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kata ya Igoma Mtaa wa Kabeke.

Mhe, Mabula akijibu maswali (32) aliyoulizwa katika mkutano huo mengi yake yakiwa ni uhaba wa Maji, Mhe. Mabula amewaomba wananchi waendelee kuwa na imani na serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Magufuli kwa kuwa una dhamira ya dhati kutatua changamoto zao ikiwemo ya ukosefu wa maji.

Mhe. Mabula amefafanua kuwa Nyamagana inategemea chanzo kimoja cha Maji cha Capripont ambacho kinaweza kuwahudumia watu 115,000 lakini kwakutambua ongezeko la watu katika wilaya ya Nyamagana ikiwa watu 1,000,000 hutegemea maji hayo asubuhi na mchana na wakazi takriban 400,000 kutegemea chanzo hicho jioni ambacho kiuhalisia hakitoshelezi.

Kwa msingi huo serikali ya CCM kwa wilaya ya Nyamagana pekee imepokea miradi mikubwa miwili ya Maji itakayo gharimu takribani 92 BIL ikiwa 75 BIL imeelekezwa katika ujenzi wa chanzo kipya Cha Maji Butimba kitakacho maliza upungufu wa maji kwa miaka 20 ijayo na tayari mkandarasi wa mradi amepatikana. Ambapo sh. 17 BIL kutengeneza tank kubwa la maji lenye uwezo wakubeba lita 2,000,000 zitakazo hudumia maeneo ya pembezoni ikiwemo Igoma, Kishiri, Luchelele, Lwanimah, Buhongwa pamoja na maeneo jirani ya wilaya tatu ifikapo mwaka 2020. Tayari mkandarasi amepatikana na wiki iliyopita serikali kupitia MWAUWASA pamoja company ya China CCECC China Civil Engineering Constration Corporation wali saini mkataba kuanza kazi mara moja.

Mhe. Mabula aliambatana na Mwenyeji wake Diwani Kata ya Igoma Mhe. Magabe, Diwani Viti Maalum Akifa Mhere, Mwenyekiti wa Fursa Community Ahmed Misanga, Mjumbe Mkutano Mkuu Taifa Mashashi pamoja na Mtendaji wa Kata, na viongozi wa jeshi la Polisi.


Share.

About Author

Leave A Reply