Sunday, August 18

RAIS JONG KIM KUKUTANA NA PUTIN NCHINI URUSI MWEZI HUU

0


Moscow, RUSSIA.

Rais Korea Kaskazini, Kim Jong Un, anatarajiwa kufanya ziara nchini Urusi na kuwa na mkutano wa kilele na Rais Vladmir Putin mapema Alhamisi wiki mjini Vladivostok mji wa pili nchini humo.

Ripoti ya gazeti moja la Urusi limezinukuu duru mbili zinazosema kuwa viongozi hao watakutana Aprili 25 mjini Vladivostok.

Wachambuzi wengi wa masuala ya siasa wanasema ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Kim kutafuta uungwaji mkono wa mataifa ya kigeni kwa ajili ya mipango yake ya maendeleo.

Itakumbukwa kuwa baada ya kuvunjika kwa mkutano wa pili wa kilele kati ya Marekani na Korea Kaskazini mjini Hanoi Februari mwaka huu kulisababisha kukwama mazungumzo na Marekani kuhusu kuondolewa vikwazo vilivyowekewa Korea Kaskazini.

Hata hivyo, Ikulu ya Urusi haijatoa maelezo kamili kuhusu mkutano huo, lakini msemaji wa serikali, Dmitry Peskov, aliwaambia wanahabari jana kuwa Putin na Kim watakutana mwishoni mwa Aprili.


Share.

About Author

Leave A Reply