Sunday, August 18

POMPEO:CIA TULIKUWA NA KOZI MAALUM YA KUSEMA UONGO NA KUTAPELI

0


New York, MAREKANI.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ambaye zamani alikuwa Mkuu wa Shirika la Kijasusi la nchi hiyo CIA, Mike Pompeo, amesema kuwa shirika hilo lilikuwa na kozi maalumu ya kufundisha watu kusema uongo na kutapeli na kusisitiza kuwa hiyo ni katika kujilinda kwa Marekani.

Waziri Pompeo alisema hayo hivi karibuni mbele ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha A & M mjini Texas na kusema wakati akizungumzia namna ya kuweka mezani sawa baina ya ukosoaji na kulegeza misimamo katika uhusiano na tawala kama za Saudi Arabia kwamba, kazi ya udiplomasia ni nzito sana.

Pombeo amesema ugumu wa kazi hiyo hauhusiani na wizara ya mambo ya nje tu bali kazi yoyote ile ikiwemo ya mkuu wa Shirika la Kijasusi la CIA ni nzito.

Aidha, ametangaza bila kificho kwamba kulikuwa na kozi maalumu ya kufundisha watu kusema uongo, kuiba na kufanya ulaghai na utapeli ndani ya CIA.

“Wakati nilipokuwa mkuu wa CIA, tulikuwa tukisema uongo, tukifanya utapeli, tukiiba. Sisi tulikuwa na kozi kamili maalumu ya namna ya kufanya mambo hayo.” Alisema Pompeo.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani vile vile amesema, yote hayo yanaonesha utukufu na hadhi ya Marekani na kubainisha kuwa uhusiano wa Marekani na nchi za dunia ikiwemo Saudi Arabia ni tofauti.

Ijapokuwa vyombo rasmi vya habari vya Marekani vimeficha na havikuipa umuhimu habari hiyo, lakini mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari vimekasirishwa mno na matamshi hayo ya Pompeo. Baadhi yao wameandika kuwa, Pompeo amethibitisha kwa ulimi wake kwamba kaulimbiu ya CIA ni kusema uongo, utapeli na kuiba.


Share.

About Author

Leave A Reply