Saturday, August 24

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWATAKA VIJANA UBUNGO KUCHANGAMKIA FURSA MBALIMBALI ZA KIUCHUMI

0


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewataka Vijana wa Wilaya ya Ubungo kuchangamkia fursa za kiuchumi kupitia uundwaji wa Vikundi,SACCOS na Makapuni ya Vijana ili kujiongezea wigo mpana wa kushiriki katika shughuli mbalimbali za
Kiuchumi.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo jana katika Ukumbi wa Urafiki Social wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya UBUNGO YA KIJANI inayoratibiwa na Umoja wa Vijana CCM(UVCCM) Mkoa wa Dar es salaam chini ya Mwenyekiti Mussa Kilakala,ambapo aliwasihi Vijana wa CCM kuwa mstari wa mbele kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kunufanika na mikopo kupitia Halmashauri na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa lengo la kukuza vipato vyao na kupunguza changamoto ya ukosefu wa Ajira.

“Zipo Kampuni za Vijana hivi sasa zimeanza kunufaika na fursa hii kutoka Serikalini,tuna Kampuni za Vijana zaidi ya 3 ambazo zimepewa tenda ya zaidi ya Tsh 2Bn kutoa mafunzo ya kilimo cha mboga mboga kupitia kitalu nyumba(Greenhouse) katika Halmashauri zote nchini.Huu ni mfano mzuri wa Serikali kuunga jitihada za Vijana kujiajiri”Alisema Mavunde

Aidha Mavunde pia aliwataka Vijana hao wa CCM kuwa mstari wa mbele kuhakikisha Chama kinashinda katika chaguzi za serikali za mitaa mapema mwaka huu Uchaguzi mkuu wa mwakani na kuwapongeza Viongozi wa CCM Mkoa na Wilaya kwa mikakati mizuri waliyojiwekea kurudisha heshima ya CCM mkoa wa Dar es Salaam.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Comrade Mussa Kilakala ameahidi kuwasimamia Vijana wa Dar es salaam katika kuzichangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi ili kupunguza tatizo la Ukosefu wa Ajira na kipato miongoni mwa Vijana,Aidha Mwenyekiti huyo pia ameuhakikishia umma wa wanaCCM kwamba kutokana na mipango na mikakati waliyojiwekea kampeni hii ya KUIKIJANISHA DAR ES SALAAM itaanza kuleta matokeo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na kumalizia mwaka 2020.


Share.

About Author

Leave A Reply