Thursday, August 22

MAMA AZINDUKA BAADA YA KUPOTEZA FAHAMU KWA MIAKA 27

0


Al Ain, SAUDI ARABIA.

Mwanamke mmoja kutoka Umoja wa falme za kiarabu (UAE) aliumia sana katika ajali ya gari iliyotokea mwaka 1991 na kupoteza fahamu lakini sasa amestaajabisha wengi baada ya kuamka kutoka kwenye koma iliyomchukua miaka 27 akiwa amepona.

Bi Munira Abdulla, alipata ajali akiwa na umri wa miaka 32 na kupata jeraha katika ubongo. Munira alipa ajali kwa kugongwa na basi wakati akiwa anaelekea kumchukua mtoto wake shuleni.

Mtoto wake Omar Webair, alikuwa na umri wa miaka minne wakati yeye na mama yake walipopata ajali. Katika ajali hiyo Omar ambaye alikuwa ameketi katika kiti cha nyuma hakujeruhiwa hata kidogo na alikutwa akiwa amekumbatiwa na mama yake.

Bi Abdulla alijeruhiwa vibaya lakini mwaka jana akiwa hospitali moja Ujerumani alianza kurudisha fahamu. Kijana wake Omar ameweka wazi kuhusu ajali walioipata na kuelezea utaratibu wa matibabu ya mama yake yaliyochukua miaka mingi.

“Alinikumbatia ili nisiumie, sikuwahi kukata tamaa kwa sababu kila siku nilihisi kuwa kuna siku mama yangu ataweza kuamka,

“Sababu kubwa ambayo imemfanya asimulie mkasa uliomkuta mama yangu ni kutaka kuwaambia watu kuacha kukata tamaa kwa watu wanaowapenda na mtu akifikia hatua hiyo haimaanishi kuwa amekufa.” Omar alisema

“Mama yangu alikuwa amekaa na mimi katika kiti cha nyuma, na alipoona tunakaribia kupata ajali, alinikumbatia ili kuniokoa katika ajali hiyo.”

Katika ajali hiyo Omar hakuumia bali alibaki na jeraha dogo kichwani lakini mama yake ambaye aliumia alichelewa kupata matibabu kwa saa kadhaa.

Miaka aliyotumia kupata matibabu.

Bi. Abdalla alifikishwa hospitali baada ya muda wa saa kadhaa kupita na baadae alihamishiwa mji wa London, huku wakusema atakuwa amepoteza fahamu lakini alikuwa ana uwezo wa kuhisi maumivu.

Baada ya muda alirudishwa katika mji wa Al Ain katika umoja wa falme za kiarabu, ambako alikuwa akiishi na mtoto wake Omar, na kuendelea kuzunguka katika vituo mbalimbali vya afya kulingana na bima aliyokuwa nayo.

Alikuwa anakula kwa mrija na kumfanya aendelee kuishi na mara kwa mara alifanyiwa mazoezi na vipimo vya viungo ili kuhakikisha kuwa misuli yake haidhoofiki kwa kuwa alikuwa hatembei.

Mwaka 2017, familia yake iliweza kupokea msaada wa fedha kutoka serikalini ili kumwezesha bi.Abdulla na hatimaye alikwenda Ujerumani kwa ajili ya matibabu.

Alifanya upasuaji mara kadhaa ili kurekebisha mkono wake uliopunguzwa na kuweka sawa, misuli ya mguu, na alipewa dawa ili kuboresha hali yake, ikiwa ni pamoja na kuamka kwake.

Kelele za hospitalini
Baada ya mwaka mmoja, siku moja mtoto wake alikuwa anajibizana ndani ya chumba cha mama yake hospitalini na kulichochea mama huyo kuamka.

“Kulikuwa na kutoelewana katika chumba alichokuwa amelazwa na alihisi kuwa niko hatarini, jambo ambalo lilimfanya ashtuke. Alihangaika kutoa sauti na nilikuwa nahangaika kuita madaktari ili wampime na walisema kuwa kila kitu kilikuwa sawa.

“Siku tatu baadae, niliamka nikasikia mtu ananiita kwa jina langu. Alikuwa ni yeye, alikuwa anaita jina langu, nilikuwa kama ninapaa kwa furaha .Kwa miaka mingi nilikuwa nikiota siku hii ifike na jina langu lilikuwa neno la kwanza kulitamka baada ya miaka 27”. Omar alisema.

“Na baadae akawa anaweza kuwasiliana na sasa baada ya maumivu ya muda anaweza kuzungumza.” Omar aliongeza.

Bi. Abdalla ameweza kurudi Abu Dhabi, ambako anaendelea kupata tiba ya viungo kwa mazoezi na kupata ushauri hasa wa namna ya kukaa na kufanya misuli kuwa imara.

Kesi kama ya Munira huwa inajitokeza mara chache.

Kuna kesi chache sana za watu kupona baada ya kupoteza fahamu kwa miaka mingi na kuendelea kuwa wazima kabisa.

Watu ambao wanapata hali hiyo na kurudi kwenye ufahamu wao baada ya koma ya muda mrefu mara nyingi tatizo lao huwa linatokana na madhara katika ubongo.

Bingwa wa zamani wa mashindano ya magari duniani, Michael Schumacher aliwahi kupata koma baada ya kupata ajali mwaka 2013 huko Ufaransa . Alipoteza fahamu kwa muda wa miezi sita kabla hajarudishwa kwao Switzerland kuendelea na matibabu.

Share.

About Author

Leave A Reply