Tuesday, August 20

KUNDI LA KIGAIDI LA DAESH (ISIS) LIMETANGAZA KUHUSIKA NA MASHAMBULIZI YA SRI LANKA

0


Colombo, SRI LANKA.

Kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) limetangaza kuwa ndilo lililohusika na milipuko ya mabomu ya hivi karibuni nchini Sri Lanka, milipuko iliyoua mamia ya watu.

ISIS imeyasema hayo leo Jumanne kupitia shirika lake la habari za kipropaganda la Amaq, ijapo kundi hilo halijatoa maelezo ya kina wala ushahidi wowote wa kuonesha kuwa ndilo lililohusika na hujuma hizo.

Hii ni katika hali ambayo, vyombo vya usalama nchini humo vimeripoti kuwa, mashambulio hayo ya Jumapili iliyopita yalifanywa na magenge ya kigaidi ya nchi hiyo.

Aidha, wapelelezi nchini humo wanasema wanachunguza iwapo waliotekeleza hujuma hizo za kigaidi wana uhusiano wowote na mitandao ya kimataifa

Huku hayo yakiarifiwa, idadi ya watu waliopoteza maisha katika hujuma hizo za kigaidi nchini Sri Lanka imeongezeka na kufikia watu 321.

Msemaji wa polisi nchini Sri Lanka amesema hadi sasa watu 500 wamethibitishwa kujeruhiwa katika mashambulizi hayo za kigaidi, ambayo yalilenga makanisa matatu, hoteli nne za kifahari na nyumba.


Share.

About Author

Leave A Reply