Thursday, August 22

KATIBU MKUU CCM TAIFA ATOA MAELEKEZO MAZITO WIZARA YA KILIMO, ADAI UHARAKISHWAJI SERA YA KILIMO

0


Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi taifa Mhe. Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amefanya ziara ya kikazi wilayani Nyamagana kutembelea ghala pamoja na kiwanda cha uchakataji mazao mchanganyiko ya nafaka Kata ya Mkuyuni na Butimba vyenye thamani ya Sh. 20. Bil.

Mhe Dkt. Bashiru akikagua ghala na kiwanda hicho ameitaka Bodi ya Mazao Mchanganyiko kuanza uzalishaji mara moja kwa kuzingatia utoaji wa bidhaa zilizoongezewa thamani ya lishe bora, kwa uzalishaji ulikuwa umesitishwa takribani miaka 21 iliyopita.

Kadhalika Mhe. Dkt. Bashiru ameshangazwa na utitiri wa bodi mbalimbali za Mazao zisizokuwa na tija ya kuwainuwa wakulima bali kuwanyonya na kuwafilisi, hivyo ameelekeza wizara ya Kilimo kuharakisha mchakato wa uundwaji Sera ya Kilimo yenye dhima ya kusaidia mkulima na sio kunufaisha wachuuzi na walanguzi. Amehimiza Wizara kuwa na Bodi mbili jumuishi nasio utitiri wa bodi zisizokuwa na tija.

Ziara hiyo imehudhuriwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Philis Nyimbi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mazao ya nafaka mchanganyiko Mhe. Monica Bega, Uongozi wa NSSF, kamati ya siasa mkoa wa Mwanza ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Dkt. Dialo, Kamati ya Siasa wilaya ya Nyamagana ikiongozwa na Katibu wa CCM wilaya Ndg. Solomon Kasaba, Mwenyekiti wa taasis ya First Community Organisation Ndg. Ahmed Misanga, Katibu wa Mbunge Jimbo la Nyamagana Bi. Florah Magabe pamoja na Diwani Kata ya Mkuyuni Mhe. Donata Gapi.


Share.

About Author

Leave A Reply