Saturday, August 17

GARI LA WANAJESHI LAGONGA MGODI NCHINI NIGER, WATANO WAFARIKI DUNIA

0


Niamey, NIGER.

Askari watano wameripotiwa kufariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari moja la kijeshi kugonga mgodi mmoja katika wilaya ya Tahoua, kaskazini mwa Niger.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, katika eneo la Tahoua sehemu ya mpaka wa Mali, gari hilo la kijeshi limeripotiwa kugonga mgodi.

Kuanzia mwezi Machi 2017, Tahoua imekuwa katika hali ya dharura, ambapo serikali ya Niger ilitangaza hali ya dharura katika maeneo karibu na mpaka wa Mali kwa sababu ya mashambulizi ya makundi ya kigaidi.

Aidha, tangu mwaka 2013 sehemu hiyo ya kaskazini ya Niger imeshuhudia mashambulizi ya vikundi vya kigaidi vinavyopigana nchini Mali na Burkina Faso.


Share.

About Author

Leave A Reply